1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Milio ya risasi yasikika Cairo

5 Februari 2011

Milio ya risasi ilisikika jana katika uwanja wa Tahrir kwenye mji mkuu wa Misri, Cairo, eneo ambalo maandamano ya kupinga utawala wa miaka 30 wa Rais Hosni Mubarak yanafanyika.

https://p.dw.com/p/10BCS
Waandamanaji wakiwa kwenye uwanja wa Tahrir Cairo, MisriPicha: AP

Taarifa hizo ni kwa mujibu wa mwandishi habari wa shirika la habari la AFP. Imeelezwa kwamba hakukuwa na taarifa za haraka zilizopatikana kuhusu majeruhi, licha ya zaidi ya watu 10,000 kimiminika usiku katika uwanja huo wakitaka Rais Mubarak aondoke madarakani, bunge jipya na kutangazwa kwa serikali ya mpito.

Baada ya sala ya Ijumaa na mapumziko, maelfu ya watu kutoka kila rika walifurika kwenye uwanja huo hapo jana katika maandamano yaliyopewa jina ''Siku ya kuondoka Hosni Mubarak.''

Kwa siku 11 mfululizo maandamano yamefanyika katika uwanja huo wa Tahrir, maandamano ambayo yametikisa nguzo za utawala wa miongo mitatu wa Rais Mubarak.

Mwandishi: Grace Patricia Kabogo (AFP)
Mhariri: Sekione Kitojo