1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Minski. Rais wa Belarus yuko Russia kujadili kuhusu bei ya gesi.

30 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCf6

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko amesema kuwa nchi yake haitapiga magoti kwa kile anachokiita kushikwa mateka na Russia katika mzozo wa bei ya gesi.

Lukashenko yuko nchini Russia kwa mazungumzo yenye lengo la kutatua mzozo huo.

Kampuni la kuuza gesi nchini Russia la Gazprom limetishia kusitisha upelekaji wa gesi nchini Belarus mwanzoni mwa mwaka mpya iwapo serikali ya nchi hiyo haitakubaliana na hatua hiyo ya kupandisha bei ya gesi.

Belarus inadai kuwa inapaswa kulipa bei ile ile ambayo Russia inalipa.

Wakati huo huo , wakaazi wa Belarus wanajitayarisha na hatua ya kukata usambazaji wa gesi hiyo iwapo utatokea siku ya Jumatatu.

Viwanda na biashara nyingine zinazotumia gesi nyingi zitakuwa za kwanza kukatiwa.

Hifadhi ya gesi hiyo ambayo inaweza kutumika kwa muda wa wiki mbili itatumika kuhudumia kuleta joto katika majumba.