1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MIRANSHAH PAKISTAN:Washukiwa wa ujasusi wakatwa vichwa na wanamgambo

26 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBMT

Wapiganaji wanaoungwa mkono na kundi la wanamgambo wakitaliban nchini Pakistan wamewakata vichwa watu wawili waliowashuku kuwa ni majasusi wanaowafanyia kazi vikosi vya wanajeshi wa Marekani nchini Afghanstan.

Miili ya watu hao ilikutikana imetupwa karibu na barabara huko Miransha ambao ni mji mkubwa mkuu wa eneo la kaskazini la Wazistan.

Watu hao inadaiwa kuwa ni mkimbizi wa Afghanstan na kiongozi wa kikabila wa Pakistan:

Wapiganaji katika eneo hilo la kaskazini na kusini mwa Waziristan wamewauwa watu kadhaa ambao wanadaiwa kuunga mkono serikali ya Pakistan au kuwachunguzia mambo wanajeshi wa Marekani wanaoongoza vita katika nchi jirani ya Afghanstan.

Eneo la Wazistan linajulikana kuwa tete na ghasia zimeongezeka tangu wanamgambo walipovunja makubaliano ya amani na serikali mwezi July.