1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miripuko Baghdad

3 Agosti 2008
https://p.dw.com/p/EpGl

Baghdad:

Kumetokea mlolongo wa miripuko ya mabomu katika mji mkuu wa Irak Baghdad mapema leo ikiwauwa watu 12 na kuwajeruhi wengine wapatao 31.Duru za serikali zilisema katika tukio baya zaidi , lori moja dogo lililoegeshwa karibu na ofisi ya uhamiaji kaskazini mwa Baghdad watu 12 waliuawa na wengine 20 kujeruhiwa. Mripuko huo mkubwa uliyaharibu pia majengo ya karibu.

Wakati huo huo katika mtaa wa Palestina katikati ya Baghdad, bomu lililotegwa kandoni mwa barabara liliwajeruhi watu 9 wakiwemo raia sita, wakati gari ya polisi wa doria ilipokua ikipita kwenye barabara hiyo.

Shambulio la tatu katika eneo la Al-Ghadir ,kusini mashariki mwa mji huo mkuu ambalo linafikiriwa lilipangwa kuyalenga magari ya serikali, liliwajeruhi raia wawili.