1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waripuaji wa kujitoa mhanga waliohusika walikwa wanawake.

29 Machi 2010

Wasafiri laki tano walikuwa kwenye treni za Moscow wakati wa miripuko, wakati wa msongamano wa watu asubuhi.

https://p.dw.com/p/Mgmd
Wasafiri waamua kutembea baada ya miripuko ya leo asubuhi mjini Moscow.Picha: AP

Walioshuhudia miripuko hiyo walisema hali ya wasiwasi ilikuwa imetanda katika vituo vya treni ambapo miripuko hiyo ilitokea na kukawa wingu la moshi na vumbi. Watu 37 wamefariki na wengine 65 wamejeruhiwa.

Hakuna kundi lolote ambalo limejitokeza kudai kuhusika na miripuko hiyo inayotajwa kama mbaya zaidi mjini Moscow kwa kipindi cha miaka sita iliyopita ingawa wanamgambo wa kaskazini mwa Urusi wanatuhumiwa.

Bomu la kwanza liliripuka katika bogi la pili la treni muda mfupi kabla ya saa mbili asubuhi kabla treni hiyo isimame katika kituo cha Lubyanka kilichoko karibu na makao makuu ya idara ya ujasusi ya Urusi, FSB na kusababisha vifo vya watu 23.

Msemaji wa wizara ya mambo ya dharura alisema mripuko mwingine ulitokea dakika 40 baadaye katika bogi la pili la treni lililokuwa katika kituo cha Park Kultury na kusababisha vifo vya kiasi ya watu 14.

Russland Zahlreiche Tote bei U-Bahn-Explosionen in Moskau‎
Polisi katika bustani la utamaduni, karibu na eneo la miripuko, Moscow.Picha: AP

Viongozi nchini Urusi wametangaza ushindi dhidi ya wanamgambo wa Chechen waliopigana vita viwili na Urusi na ingawa ghasia zimepungua Chechnya, zimesambaa na kutokota zaidi katika maeneo ya Dagestan na Ingushetia ambapo mapigano ya kiukoo yanapishana na matukio ya genge za uhalifu na wanamgambo wa Kiislamu.

Meya wa mji wa Moscow, Yuri Luzhkov aliwaambia waandishi wa habari kwamba waripuaji wawili wa kujitoa mhanga waliohusika walikuwa wanawake. Kiongozi wa mashtaka alisema wameanzisha uchunguzi wa ughaidi baada ya wataalam wa idara inayotafuta ushahidi kupata mabaki ya mwanamke katika vifusi.

Dhamana ya sarafu ya Rouble ya Urusi ilishuka kwa kiwango cha nukta 12 kutoka 34.25 kwa kipindi cha asubuhi dhidi ya sarafu za Euro na Dola kutokana na hofu kwamba miripuko hiyo inaashiria mwanzo wa msururu wa miripuko katika miji ya Urusi.

Kulingana na duru katika uongozi wa Kremlim katika mahojiano na shirika la habari la Reuters, rais wa Urusi, Dmitry Medvedev atatoa taarifa kwa taifa baadaye leo. Waziri mkuu Vladmir Putin pia anafuatilia matukio hayo.

Russland Zahlreiche Tote bei U-Bahn-Explosionen in Moskau‎ NO FLASH
Maafisa wa uokozi katika kituo cha Lubyanka mjini Moscow.Picha: AP
Russland Wahlkampf Dmitry Medvedev
Rais wa Urusi, Dmitry Medvedev kuhutubia taifa baadae leo.Picha: AP

Idadi ya waliofariki inaifanya miripuko hiyo kuwa mbaya zaidi tangu mripuko wa mwaka 2004 uliotokea mjini Moscow wakati mripuaji wa kujitoa mhanga kusababisha vifo vya watu 39 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 100 katika treni.

Wanamgambo wa Chechen wanaluamiwa kwa miripuko hiyo na shauku kubwa ni katika eneo la kaskazini ambapo kiongozi wa waasi, Doku Umarov anapigania kudhibiti eneo la Kiislamu na aliapa mwezi Februari kuendeleza vita vyake katika miji ya Urusi.

Alipohojiwa katika mtandao wa Kiislamu alisema damu haitamwagika tu katika eneo lao bali vita vitakuwa katika miji ya Urusi.

Mwandishi, Peter Moss, Reuters, DPA/ AFP

Mhariri, Othman Miraji