1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misaada yawafikia wahanga kwa taabu ,Ufilipino

Abdu Said Mtullya13 Novemba 2013

Misaada ya kimataifa imeanza kuwafikia watu waliokumbwa na maafa ya kimbunga Haiyan katika kisiwa cha Ufilipino lakini mwandishi wetu Peter Hille anasema kwamba watoaji misaada wanakabiliwa na matatizo

https://p.dw.com/p/1AGM6
Misaada kutoka Ujerumani yawasili Ufilipino
Misaada kutoka Ujerumani yawasili UfilipinoPicha: picture-alliance/dpa

Maalfu kwa maalfu ya watu wanataka kuondoka kwenye vijiji na miji iliyokumbwa na kimbunga Haiyan kutokana na ukosefu wa huduma za lazima kama vile maji na chakula na hofu ya kuporwa kwa mali za watu pia inadizi kuwa kubwa. Njia za kuwafikia watu wanaohitaji misaada zimefunikwa na vifusi.Sehemu nyingi hazipitiki.

Mawasiliano yakatika

Jimbo la Tacloban ni mojawapo ya sehemu zilizoathirika sana na maafa yaliyosababishwa na kimbunga Haiyan. Meredith Dumdum anatokea katika jimbo hilo kwa sasa yupo kwenye uwanja wa ndege wa Cebu mashariki mwa kisiwa cha Ufilipino .Amekusanyika na watu wengine kwenye uwanja huo.Familia yake ilikuwa katika jimbo la Tacloban, maafa yalipotokea .

Amesema eneo lote ,limefagiliwa na amaeeleza kuwa hana habari zozote juu ya watu walioko huko.Kwa sasa Meredith hana mawasiliano na watu wake. Ni binamu yake tu aliemipigia simu mara moja.Bado anasubiri simu nyingine.Meredith amejaribu kuwasiliana na jamaa zake katika jimbo la Tacloban bila ya mafanikio.

Miundombinu yateketezwa

Kimbunga Haiyan kimezitekeleza sehemu nyingi na kusababisha kukatika kwa mawasiliano. Barabara nyingi zimefunikwa na miti iliyong'oka na kuanguka kutokana na nguvu ya kimbunga. Hata hivyo watoaji misaada ,hatua kwa hatua wanazifikia sehemu zilizoathirika kwa kiwango kikubwa. Watoaji misaada hao wanapitia uwanja wa ndege wa Cebu. Waokozi na shehena zao za misaada wanafika katika mji wa Cebu kwa ndege wakiwa tayari kuelekea katika sehemu za maafa..

Watoaji wa misaada wanafika na vifaa vya tiba na mashine za kusafishia maji. Lakini wananakabiliwa na matatizo kuhusu njia ya kuvifikisha vitu hivyo katika sehemu za maafa. Pia pana tatizo kwenye uwanja wa ndege wa Tacloban.Hali ya mapokezi huko siyo nzuri. Uwanja wa ndege wa Tacloban umeharibika sana kutokana na nguvu ya kimbunga na njia kuendea mjini kutoka kwenye uwanja huo pia inapitika kwa taabu. Lakini watoaji misaada wanatumai kwamba watafanikiwa kufika katika jimbo la Tacloban hapo kesho.

Ujerumani yaongeza msaada wa fedha kwa Ufilipino

Wakati huo huo Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle amesema mjini New Delhi kuwa Ujerumani imeongeza msaada wa fedha kwa Ufilipino hadi Euro Milioni moja na nusu.

Mwandishi: Hille Peter,

Tafsiri:Mtullya Abdu.

Mhariri: Josephat Charo