1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misri magazetini nchini Ujerumani

14 Februari 2011

Mustakbal wa Misri baada ya kung'oka madarakani Hosni Mubarak ndiyo mada iliyohanikiza magazetini humu nchini hii leo

https://p.dw.com/p/10Gp0
Bango lililochorwa na mwanaharakati wa kike wa MisriPicha: dapd

Tuanzie Misri ambako wahariri wanakubaliana kuondoka madarakani Mbarak ni hatua ya mwanzo na ndogo tuu-yaliyosalia ndio mengi na makubnwa.Gazeti la "Hessische/Niedersächsischer Allgemeine linaandika:

Siku moja tuu baadae,ilidhihirika kwamba Mubarak kung'oka madarakani ilikuwa hatua ndogo tuu ikilinganishwa na njia ndefu na tete ambayo Misri inabidi kuifuata hivi sasa:katiba inabidi idurusiwe,vyama vya kisiasa vinahitaji kurekebisha muongozo wao na uchaguzi huru unabidi kuitishwa.Lawama dhidi ya Mubarak ndizo zilizowaunganisha waandamanaji-sasa ndio mivutano itaanza kuibuka.Demokrasia ina utaratibu maalum wa maridhiano ambao wamisri hawakupata nafasi bado ya kujifunza.Na katika njia yao ya kuelekea katika mustakbal mwema,wanaweza kujikuta wakivunjika moyo au hata kukwama.Na sauti hazitakawia kuhanikiza,watu wakihoji-sio yote ya Mubarak yalikuwa mabaya-angalao watu walikuwa na utulivu."

Gazeti la "Rhein-Necker-Zeitung lina maoni sawa na hayo na linaandika:

"Mubarak ameshang'oka madarakani.Hata hivyo ukichunguza kwa makini hutakosa kugunduwa katika nchi ya mafirauni hakuna mengi yaliyobadilika.Wengi wanahisi kinyume chake.Waandamanaji wameridhika,wanavunja mahema na kusubiri mageuzi.Wanajeshi hawapotezi wakati, wanabuni utaratibu mpya wa uongozi-lakini kama utaratibu huo utageuka kuwa mfumo wa demokrasia katika kipindi kifupi kijacho au kama wenye maguvu wataendelea kupora mali ya nchi hiyo-ni suala la kusubiri na kuona."

Na gazeti la "Financial Times"(Deutschland) linaandika:

Maajabu mengine yatatokea pale wanajeshi watakapoamua kuwakabidhi raia na kwa njia za kidemokrasia madaraka waliyojipatia kutokana na kilio cha wananchi.Nchi za Ulaya na Marekani wanabidi wafanye kila liwezekanalo kuhakikisha jambo hilo.Hilo litawezekana tuu ikiwa katika kutathmini utulivu na demokrasia,wezani utaelemea zaidi upande wa demokrasia.Ulaya na Marekani hawastahiki kufanya kosa na kuwaachia wamsiri wenyewe utulivu ambao bado si imara.Wanabidi wafikirie namna ya kuwasaidia kiuchumi na kuhakikisha uchaguzi unaitishwa kama ilivyopangwa msimu wa mapukutiko ujao.

Flash-Galerie Bundeswehr-Einsatz in Afghanistan
Mwanajeshi wa Ujerumani nchini AfghanistanPicha: AP

Na hatimae magazeti ya Ujerumani yamechambua pia pendekezo la kuwafungulia milango wageni wajiunge na jeshi la shirikisho Bundeswehr.Gazeti la Oldenburgische Volkszeitung linaandika:

"Kuruhusiwa wageni wajiunge na jeshi la shirikisho Bundeswehr ni dalili nyengine ya mageuzi ya kina.Mwishoe utaratibu huo utapelekea kuwepo jeshi la waajiriwa.Hali hiyo sio tuu inaingia akilini lakini pia ni ya maana.Kwasababu jukumu la jeshi la shirikisho tangu lilipoanzishwa May tano mwaka 1955 limeongezeka pakubwa.Wanajeshi wa Ujerumani wanawajibika hivi sasa nchi za nje na katika opereshini za kivita pia wanashiriki.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir:Inlandspresse

Mpitiaji:Yusuf Mwasimba Saumu