1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misri yaimarisha hatua kuzuwia wahamiaji kuingia Israel

30 Julai 2009

Risasi zatumika dhidi ya wanaotaka kuvuka mpaka.

https://p.dw.com/p/J0K5
Wahamiaji wakiwa safarini katika kiu cha kuvuka kuingia Israel au UlayaPicha: AP

Misri imeimarisha hatua yake ya kuwapiga risasi wahamiaji wa kiafrika wanaojaribu kuvuka mpaka kuingia Israel. Kumiminikia wahamiaji hao Israel, ni ishara ya mabadiliko katika suala zima la kiu cha wahamiaji barani Afrika cha kutafuata maisha bora nje ya bara hilo. Matumizi hayo ya nguvu ni ishara kubwa ya mabadiliko katika suala hilo la wahamiaji wa kiafrika kutoka nchi zilizoko kusini mwa Misri. Idadi kubwa zaidi ya wanaotafuta uwezekano wa kuingia Israel ni kutoka Eritrea. tangu mwezi Mei mwaka huu polisi wa Misri wamewapiga riasasi na kuwaua kiasi ya wahamiaji sita wakiafrika, katika kile polisi inachosema ni kujibu kile inachokiita kuwa ni ongezeko biashara haramu ya binaadamu.Njia hiyo ya kujaribu kuingia Israel kwa kupitia Misri inatokana na mazingira kuwa magumu nchini Libya iliokua ikitumiwa kama njia ya kusafiri kimagendo kuingia Ulaya.

Pia ni jitihada ya Polisi wa Misri kuwazuwia pia wenye azma ya kuingia Ulaya ambapo nchi kadhaa zimeimarisha maamuzi yao ya kisiasa kuhusiana na suala hilo, hasa katika wakati huu wa msukosuko wa kiuchumi duniani.

Maafisa wa shughuli za misaada wameieleza njia wanayopitia wahamiaji huko Misri kuwa sawa na mto wa vyonzo viwili, ukianzia pembe ya Afrika na wahamiaji wa kiuchumi na wakimbizi huku baadhi wakiukimbia utawala wa kiimla nchini Eritrea na wakimbizi kutoka jimbo la magharibi mwa Sudan la Darfur.

Changa moto inayowakabili sasa ni ama kukabiliana na ufyatuaji risasi katika mpaka wa Misri na Israel au kujaribu bahati yao kwa njia ya usafiri wa baharini nchini Libya kuingia Ulaya na kuikabili hatari ya kuzama. Mkuu wa ofisi ya wakimbizi ya Umoja wa mataifa mjini Kassala, mashariki mwa Sudan Mohamed Dualeh anasema taarifa alizopokea ni kuwa njia ya Libya sasa ni ngumu kwa sababu ya ukaguzi mkali katika mpaka wake na Sudan . Idadi ya wanaoingia Sudan kutoka Eritrea katika nusu ya kwanza ya mwaka huu 2009 imeongezeka mara mbili kutokana na kuwasili wahamiaji wapya 11.000, wengi miongoni mwao wakiwa na matumaini ya kuvuka kuingia Israel kupitia Misri.

Misri inahofia hali hiyo inaweza kusababisha kitisho cha usalama katika mpaka wake wa Sinai.tayari iana wasi wasi juu ya waislamu wa itikadi kali. Aidha Misri inakabiliwa pia na mbinyo wa Israel inayoitaka kuzuwia wimbi hilo la wahamiaji kuingia Israel. Misri iliokua ikiwavumilia maelfu ya wahamiaji kutoka nchi kadhaa za kiafrika mnamo miaka ya karibuni, pia iliwarudisha nyumbani mamia ya wahamiaji kutoka Eritrea licha ya upinzani wa Umoja wa mataifa ambao ulihofia wangeweza kuteswa.

Flüchtlingsschiff mit afrikanischen Immigranten aufgebracht
Mashua iliofungwa na boti ikiwa na wahamiaji haramu 44, ikisindikizwa hadi bandarini katika kisiwa cha Uhispania cha Canary.Picha: picture-alliance/ dpa

Pamoja na hayo kwa miezi kadhaa sasa hali ni shwari katika mpaka wa Misri, baada ya Libya kuidhinisha makubaliano na Itali kuwazuwia wahamiaji wanaojaribu kuingia Ulaya. Mwezi Mei Itali ilianza kuwarejesha Libya wahamiaji ambao boti zao zilizuiliwa baharini

Lakini mashirika yanayotetea haki za binaadamu yameipinga hatua hiyo yakisema mamia ya waliorejeshwa wamekabiliwa na visa vya ukiukaji wa haki za binaadamu ikiwa ni pamoja na kuwekwa magerezani.

Mwandishi: Mohamed Abdul-Rahman/Reuters

Mhariri Thelma Mwadzaya