1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misri yaitia wasiwasi ulimwengu

1 Februari 2011

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo wameyaangazia masuala kadhaa yanayogonga vichwa vya habari ndani na nje ya nchi ikiwemo,hali ya kisiasa nchini Misri,ziara ya Kansela Merkel nchini Israel na siasa kwa ujumla

https://p.dw.com/p/QxGs
Rais wa Misri Hosni Mubarak na Waziri mpya wa mambo ya ndani Mahmoud Wagdi kama ilivyoonyesha televisheni ya taifaPicha: dapd
Tuanzie na gazeti la Neue Osnabrücker na Mhariri wa gazeti hilo anaiamulika hali nchini Misri ukiuzingatia mtazamo wa mataifa ya bara la Ulaya.Ni nadra kwa mwanadiplomasia mkuu wa Umoja wa Ulaya anayehusika na masuala ya kigeni kukosa la kusema kuhusu mgogoro wowote ule duniani.Jumuiya hiyo hata hivyo ina mtazamo tofauti kuhusu purukushani zinazoendelea huko Misri.
Catherine Ashton EU-Außenbeauftragte Amr Moussa Ägypten Kairo
Amr Moussa wa Umoja wa mataifa ya Kiarabu na Bibi Catherine Ashton wa EUPicha: AP
Upi msimamo wa Jumuiya hiyo? Msimamo wa Umoja wa Ulaya ni kuyaunga mkono mageuzi yaliyo na misingi ya kidemokrasia.Tayari wameutolea uongozi wa Misri wito wa kuuheshimu uhuru wa umma kadhalika kukisikiliza kilio cha wapinzani wa serikali.Endapo hilo litatimia ustawi wa nchi utaimarika,hata hivyo hilo haliaminiki kwani waandamanaji wamejitosa majiani ili kuitimiza haki yao ya demokrasia.Kilicho bayana ni kwamba,wapinzani wa serikali ambao ni Waislamu walio na misimamo mikali pamoja na wapenda mageuzi,msimamo wao wa pamoja ni:Utawala wa Rais Hosni Mubarak ufikie kikomo,limeandika gazeti. Hatma ya Mashariki ya Kati Mhariri wa Neue Osnabrücker anaendelea kufafanua kuwa hali hiyo inalitishia eneo zima la Mashariki ya Kati.Taswira hiyo inayotisha huenda ikaziathiri harakati za kutoa misaada za Ujerumani na bara la Ulaya kwa jumla.Anasisitiza kuwa binafsi,Rais Mubarak haifahamu demokrasia na amekuwa akiiongoza nchi hiyo kwa mkono wa chuma.Kiongozi huyo hana budi ila kuwateua viongozi wapya.Kulingana na mhariri wa gazeti la Neue Osnabrücker,Misri inahitaji mageuzi yanayozingatia demokrasia na wala sio mapinduzi yanayosababisha vurugu na ghasia. Mtazamo wa Ruprecht Polenz Akizungumza na gazeti la Rheinische Post,Kiongozi wa kamati ya masuala ya kigeni katika Bunge la Ujerumani,Ruprecht Polenz alikiri kuwa raia wa Misri wana haki ya kucharuka na kudai uongozi bora.Hata hivyo jambo la kwanza na la msingi,ni kuyaandaa mazingira yanayoupa kipa umbele usawa na haki kabla ya uchaguzi kufanyika.Gazeti la Rheinischepost linaeleza kuwa,kwa mtazamo wa mwanasiasa huyo,ni bora uchaguzi ukifanyika katika kipindi cha miezi sita ijayo.
Merkel Netanjahu Deutsch-Israelische Konsultationen
Kansela Angela Merkel na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanjahu wakiwa JerusalemPicha: dapd
Ziara ya Kansela Angela Merkel ya Israel Mhariri wa gazeti la Frankfurter-Allgemeine anaanza na kuielezea ajenda kuu ya ziara hiyo ya siku mbili inayojikita katika maendeleo ya eneo la mataifa ya Kiarabu hususan Misri kwenyewe.Kulingana na mhariri huyo,azma ya Israel ni kuendelea kuwa mshirika muhimu wa nchi jirani ya Misri kwasababu za maslahi ya kijeshi na usalama wa kanda hiyo. Malengo ya kisiasa? Mhariri anafafanua kuwa ,la msingi ni:Misri ndicho kiungo muhimu kati ya Waisraeli na Wapalestina kinachoyaunganisha moja kwa moja mataifa mengine ya Kiarabu kadhalika kuwa mwenyeji wa vikao vya kimataifa vinavyoyajadili masuala ya hali nzima ya eneo la Mashariki ya Kati kila inapohitajika. Kwa kumalizia gazeti la Frankfurter Allgemeine linasisitiza kuwa,Kansela Angela Merkel huenda akanufaika na mchango wa Israel katika hali nzima ya Misri ila kwa masharti:Endapo mtazamo wa Ujerumani unabadilika. Mwandishi:Mwadzaya,Thelma-Inlands Presse Mhariri:Abdul-Rahman