1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mita 800: Rudisha avunja rekodi ya dunia

10 Agosti 2012

Mwendambio wa kasi kabisa duniani kwa sasa Usain Bolt alitimka mbio na kufanikiwa kutetea taji lake la mbio za mita 200 katika michezo ya Olimpiki akiongeza mavuno ya nchi yake Jamaica ya medali za dhahabu.

https://p.dw.com/p/15nUN
epa03353379 David Lekuta Rudisha of Kenya celebrates winning the men's 800m final at the London 2012 Olympic Games Athletics, Track and Field events at the Olympic Stadium, London, Britain, 09 August 2012. At right is Nijel Amos of Botswana who placed second. EPA/BERND THISSEN +++(c) dpa - Bildfunk+++
Bingwa wa mbio za mita 800 David RudishaPicha: picture-alliance/dpa

Usain Bolt amekuwa pia mtu wa kwanza duniani kuweza kushinda mbio za mita 100 na 200 katika msimu mmoja wa Olimpiki .Lakini la kusisimua zaidi ni pale David Rudisha wa Kenya alipovunja rekodi ya dunia katika mbio za mita 800.

Mbio hizo zimefikisha kilele siku ya kihistoria wakati David Rudisha wa Kenya alipovunja rekodi ya dunia ya mbio za mita 800, akiwaacha wakimbiaji wenzake nyuma mara tu baada ya mbio hizo kuanza.

Rudisha alikuwa akilenga kuweka historia tangu pale mbio hizo zilipoanza , akiwa mtu wa kwanza kukimbia mbio hizo chini ya dakika moja na sekunde 41. "Sikuwa na shaka yoyote na ushindi , lakini nilikuwa nasubiri mazingira maalum kuweza kuvunja rekodi hii, alisema Rudisha kwa kujiamini".

Nae mkuu wa kamati ya maandaandalizi ya michezo hiyo ya London Sebastian Coe ambaye binafsi alikuwa akishikilia rekodi ya dunia ya mbio hizo za mita 800, amesema na hapa namnukuu: "Badala ya kufanya juhudi tu za kushinda, alitaka kufanya kitu cha ziada .. ..ushindi wa Rudisha utaingia katika historia kuwa ni mmoja kati ya ushindi adhimu katika Olimpiki".

Kwa upande wake Usain Bolt muda aliotumia unafikisha muda wa nne kwa kasi katika mbio hizo wakati alipopunguza kasi katika mita 30 za mwisho, akihisi kuwa hajaweza kufikia nafasi ya kuweza kuvunja rekodi ya dunia. Medali ya fedha imekwenda kwa hasimu wake Mjamaica Yohan Blake na pia shaba ikaangukia huko huko Jamaica kwa Warren Weir. Nilijua kuwa itakuwa rekodi ya dunia nilipofika katika kona , nilikuwa nahisi hivyo, Bolt amesema. Nilitaka kwa dhati kujaribu kupata rekodi ya dunia katika mbio za mita 200 lakini ilikuwa vigumu kuliko nilivyofikiria.

LONDON, ENGLAND - AUGUST 09: Gold medalist Usain Bolt (C) of Jamaica celebrates with silver medalist Yohan Blake (L) of Jamaica and bronze medalist Warren Weir (R) of Jamaica after the Men's 200m Final on Day 13 of the London 2012 Olympic Games at Olympic Stadium on August 9, 2012 in London, England. (Photo by Stu Forster/Getty Images)
Wakimbiaji wa Jamaica Usain Bolt katikati, Yohan Blake kushoto na Warren WeirPicha: Getty Images

Hata hivyo vumbi litatimka tena leo katika mbio za mita 100 wanaume kupokezana vijiti katika kuwania kufuzu katika fainali za mbio hizo. Oscar Pistorius wa Afrika kusini mwanariadha ambaye anatumia miguu ya bandia amenyimwa nafasi ya kushiriki mbio hizo. Pia kutakuwa na michuano ya awali ya mbio za mita 400 kupokezana vijiti kwa wanawake. Pia kutakuwa na fainali ya mbio za mita 1,500 kwa wanawake, pamoja na mbio za mita 5,000 wanawake.

South Africa's Oscar Pistorius starts his men's 400m round 1 heats at the London 2012 Olympic Games at the Olympic Stadium August 4, 2012. REUTERS/Dylan Martinez (BRITAIN - Tags: OLYMPICS SPORT ATHLETICS TPX IMAGES OF THE DAY)
Mkimbiaji wa Afrika kusini Oscar PistoriusPicha: Reuters

Nae mwanariadha wa Ufaransa Hassan Hirt anayekimbia mbio za mita 5,000 amepigwa marufuku kushiriki katika mbio hizo baada ya kupatikana na hatia ya kutumia madawa ya kuongeza nguvu.

Wakati huo huo Marekani imejipatia medali ya dhahabu katika soka la wanawake baada ya kuibwaga Japan kwa mabao 2-1, katika mchezo ulioshuhudiwa na watu 80,000 katika uwanja wa Wembley jana.

Marekani imeipiku China sasa katika msimamo wa medali, ambapo sasa imefikisha medali 39 dhidi ya 37 za China.

Mwandishi : Sekione Kitojo / rtre

Mhariri: Yusuf Saumu