1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mitchell akutana na Perez

9 Juni 2009

Marekani yahimiza mazungumzo Mashariki ya kati

https://p.dw.com/p/I6Jc
Mitchell na NetanyahuPicha: AP

Mjumbe maalumu wa Marekani kwa Mashariki ya kati George Mitchell, amehimiza leo kuanzishwa upya mazungumzo ya amani baina ya wapalestina na Israel na wakati huo huo, ameihakikishia Israel, kuwa usuhuba wake na Marekani utabakii vile vile licha ya tofauti zao zilizoibuka juu ya ujenzi wa maskani ya wayahudi na kuwapo kwa dola mbili bega kwa bega.

Kwa upande mwengine,Misri nayo imekutana leo na Kiongozi wa Hamas ,Khaled Mashaal mjini Cairo katika jaribio la kumaliza mfarakano huko Ukingo wa magharibi kati ya wapiganaji wa Hamas na vikosi vya usalama vya Mamlaka ya ndani ya wapalestina inayoungwamkono na kambi ya magharibi:

Katika mazungumzo yake hii leo mjini Jeruselem na Rais Shimon Perez, mjumbe wa marekani kwa Mashariki ya kati Bw.George Mitchell alisema kuwa wote wana wajibu wa kuleta masharti ya kuanzishwa haraka mazungumzo.

Katika mvutano ulioibuka wazi hadharani baina ya washirika hao 2 wa chanda na pete-Israel na Marekani tangu kupita muongo mmoja, Rais Barack Obama na waziri mkuu Benjamin Netanyahu hawasikizani juu ya ujenzi zaidi wa maskani za wayahudi na kubisha kwa Netanyahu kuridhia kuundwa kwa dola la wapalestina litakaloishi bega kwa bega kwa amani na lile la Israel.

Waisraeli wakihofia kuwa Rais Obama anatumai kutengeneza heba ya Marekani katika macho ya waarabu kwa kukuza mvutano na Netanyahu,Bw.Mitchell amezungumza kirafiki juu ya Israel kwa maripota. Alisema,

"Niacheni nifafanue wazi.Tofauti hizi zilizozuka si mvutano kati ya maadui, kwani Marekani na Israel zinabakia kuwa washirika wakubwa na marafiki."

Bw.Mitchell akasisitiza tena kujitolea kweli kwa Marekani kuona linaundwa dola la wsapalestina likiishi bega kwa bega na Israel kwa amanai na katika hali ya usalama.

Itakumbukwa kwamba katika hotuba yake kwa ulimwengu wa kiislamu alioitoa mjini Cairo wiki iliopita, Rais Obama aliitaka Israel kukomesha kujenga

Muandishi: Ramadhan Ali

Mhariri: M.Abdul-Rahman