1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MIYEH MIYEH:Ghasia kati ya Hamas na Fatah katika kambi ya Lebanon

4 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Ig

Raia mmoja wa Palestina wa mfuasi wa chama cha Fatah amepigwa risasi na kujeruhiwa katika mapigano kati yao na kundi hasimu la Hamas kwenye kambi ya wakimbizi ya Lebanon.

Mapigano hayo yalitokea katika kambi ya Miyeh Miyeh iliyo kusini mashariki mwa mji wa pwani wa Sidon na kudumu kwa saa moja u nusu.Chama cha Fatah kinachoongozwa na Rais Mahmoud Abbas kimekuwa kikizozana waziwazi na kundi la Hamas tangu lilipoteka ukanda wa Gaza mwezi Juni.

Wakati huohuo Rais George Bush wa Marekani na kiongozi wa bunge la Lebanon Saad Hariri wanatarjiwa kufanya mazungumzo hii leo kujadilia hali nchini humo pamoja na ushawishi wa nchi jirani ya Syria.Viongozi hao wawili aidha wanatarajiwa kuzungumzia uchaguzi wa rais ujao wa Lebanon huku Marekani ikiahidi kushirikiana na kiongozi atakayeteuliwa kwa njia ya uhuru.

Mauaji ya kisiasa yamekumba Lebanon kikiwemo kifo cha Waziri Mkuu wa zamani Rafiq Hariri aliyeuawa mwaka 2005 aidha mwanasiasa anayepinga Syria Antoine Ghanem mwezi jana.Bunge la Lebanon liliahirishwa hadi Oktoba 23 kwa ukosefu wa wabunge wa kutosha kushiriki katika shughuli ya uchaguzi wa rais.