1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mizozo ya Sudan itatuliwe kwa amani

Martin,Prema24 Juni 2011

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani,Guido Westerwelle ametoa mwito kwa pande zote mbili za Sudan,kutenzua mizozo yake kwa amani. Alipokuwa Khartoum alisema, uhuru wa taifa jipya la Sudan Kusini haupaswi kutiwa hatarini.

https://p.dw.com/p/RVSs
Bundesaußenminister Guido Westerwelle (M, FDP) wird am Donerstag (23.06.2011) bei seiner Ankunft auf dem internationalen Flughafen von Khartum begrüßt. Westerwelle ist zu einem Besuch im Sudan eingetroffen. Zunächst stehen am Donnerstag Gespräche in der Hauptstadt Khartum auf dem Programm. Anschließend reist Westerwelle in die Krisenprovinz Darfur weiter sowie in den Süden des Landes, der sich im nächsten Monat für unabhängig erklären will. Foto: Thomas Trutschel dpa +++(c) dpa - Bildfunk+++ dpa 25436607
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle (kushoto) ziarani SudanPicha: picture alliance/dpa

Sudan Kusini inatazamia kutangaza uhuru wake Julai 9, wakati ambapo Ujerumani itakuwa na wadhifa wa urais katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Pande hizo mbili za Sudan zinakabiliwa na mizozo kadha ya mipaka.

Hata hivyo, zimekubaliana kuwa na eneo ambako majeshi hayatoruhusiwa katika jimbo hilo la mpakani la Abyei. Migogoro mingine inayohitaji kutenzuliwa inahusika na ugawaji wa pato la mafuta pamoja na njia ya kugawana madeni ya taifa. Waziri Westerwelle leo anatazamiwa kwenda Sudan Kusini kukutana na Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir mjini Juba.