1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mjadala wa bajeti Bungeni

Abdu Said Mtullya9 Aprili 2014

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameyatetea mageuzi katika mfumo wa pensheni yaliyopendekezwa na Waziri wake wa ajira Andrea Nahles. Kansela Merkel ameyatetea mageuzi hayo bungeni .

https://p.dw.com/p/1BeZT
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel
Kansela wa Ujerumani Angela MerkelPicha: Reuters

Akichangia katika mjadala wa bajeti ya Ujerumani kwa mwaka wa 2014 Kansela Merkel amesema Ujerumani ni miongoni mwa nchi zinazonufaika na sera ya dunia utandawazi. Bibi Merkel amefahamisha kwamba katika muhula huu kiasi cha Euro Bilioni sita kitaekezwa katika maendeleo ya elimu na utafiti.

Katika mjadala uliochukua muda wa saa nne Kansela wa Ujerumani alionekana kama alikuwa tayari kufunga kibwebwe alipomjibu mbunge wa chama cha mrengo wa shoto Katja Kipping kwa kumwambia kwamba aliyokuwa anayazungumza yalikuwa nje ya ukweli.

Serikali yakosolewa

Kiongozi wa chama cha mrengo wa shoto bibi Kipping aliliaumu serikali kwa kufuata sera isiyokuwa na manufaa ya kijamii.

Akimjibu mbunge huyo wa chama kikuu cha upinzani, Kansela Merkel amesema mawazo mazuri nchini Ujerumani hayapaswi kuwekwa kando.Kila linalopasa lazima litumike. Ameeleza kwamba ubunifu ndiyo injini ya neema nchini Ujerumani.

Wabunge wa Ujerumani wameujadili mpango wa bajeti kwa ajili ya miaka ijayo. Kansela Merkel amemsifu Waziri wake wa fedha Wolfgang Schäuble.Amesema Waziri Schäuble ameelekeza juhudi katika kuleta utengemavu wa kifedha nchini Ujerumani. Bibi Merkel amesema kutokana na juhudi za Waziri wake wa fedha, kwa mara ya kwanza tokea muda mrefu Ujerumani inakaribia kuwa na bajeti linganifu.

Merkel atahadharisha juu ya uchumi wa dunia

Bibi Merkel aliutumia muda mwingi wa hotuba yake kuzungumzia juu ya masuala ya kiuchumi. Ametahadharisha juu ya kuendelea kwa mdororo wa uchumi wa dunia.Amesema mgogoro wa madeni barani Ulaya bado haujamalizika an kwamba maendeleo katika baadhi ya nchi zenye uchumi mdogo yapo mashakani.

Hata hivyo mbunge wa chama cha mrengo wa shoto ambacho ni chama kikuu cha upinzani ,Bibi Kipping ameilaumu serikali ya mseto inayoongozwa na Kansela Merkel kwa kuzipuuza juhudi za kupambana na umasikini na kwamba serikali ya bibi Merkel iinaupora mfuko wa kijamii kwa ajili tu ya kuiweka sawa bajeti.

Lakini Kansela Merkel aljibu kwa kusema kwamba Bibi Kipping alikuwa kando ya ukweli.

Naye kiongozi wa wabunge wa chama kijani Katrin Göring - Eckardt ameikosoa serikali ya mseto ya inayoongozwa na Kansela Merkel kwa kuendesha sera zinazowaathiri, vijana masikini pamoja na mazingira.Amesema serikali hiyo ya vyama vya CDU, SPD na CSU inafanya kazi ya kuyaahirisha maamuzi muhimu. Amemkosoa Waziri wa uchumi Sigmar Gabriel wa chama cha SPD kwa kuwa mpiga debe mkubwa wa maslahi ya mameneja.

Mwandishi:Mtullya abdu.

Mhariri:Yusuf Saumu