Matukio ya Kisiasa

Mjadala wa udhibiti wa umiliki bunduki washika kasi Marekani

Chama kinachotetea umiliki wa bunduki nchini Marekani NRA chataka shirika la udhibiti wa bunduki na zana za milipuko ATF kutafakari kubadilisha sheria kuhusu vifaa vinavyoongezea bunduki uwezo zaidi.

Bump Stock Waffe USA (Getty Images/G.Frey)

Wabunge wa Marekani hapo Alhamisi waliimarisha  juhudi zao za kupiga marufuku vifaa vilivyotumiwa na mshambuliaji wa Las Vegas vilivyowezesha bunduki yake kufyatua risasi kwa haraka. Kadhalika chama cha kitaifa cha wamiliki bunduki kimewahimiza maafisa wa shirikisho kuujadili uhalali wa kisheria wa vifaa hivyo.

Bila ya kutarajiwa, Chama kinachotetea umiliki wa bunduki nchini Marekani NRA kilivunja utamaduni wake wa tangu zamani wa kuzipinga juhudi zozote za kudhibiti umiliki wa bunduki, pale kilipolitaka shirika la udhibiti wa bunduki na zana za milipuko  ATF kutafakari kubadilisha sheria .

Kwenye taarifa yake, NRA inaamini kuwa vifaa vinavyowezesha bunduki ndogo kufanya kazi kwa nguvu kubwa sawa na bunduki zenye uwezo mkubwa zinapaswa kuwekewa sheria zaidi.

Kifaa kinachounganishwa na bunduki kuipa uwezo mkubwa kufyatua risasi

Kifaa kinachounganishwa na bunduki kuipa uwezo mkubwa kufyatua risasi

White House ipo tayari kwa mjadala wa kudhibiti umiliki wa bunduki

Huku maafisa wa polisi wakichunguza kilichomsababisha Stephen Paddock kuwaua watu 58 na kuwajeruhi 500 katika tamasha la muziki mjini Las Vegas mapema wiki hii, Ikulu ya White House pia ilitangaza kuwa ipo tayari kwa mazungumzo zaidi kuhusu vifaa hivyo. Juhudi za mtangulizi wa trump, Brack  Obama kutaka udhibiti wa bunduki hazikuzaa matunda.

Hata hivyo baadhi ya Wademocrats sasa wanasema ipo haja kubwa kudhibiti umilikaji huo. Seneta wa jimbo la California Dianne Feinstein asema: "Lazima tuseme yanatosha . Lazima tuseme hakuna haja ya kuibadilisha bunduki ndogo kuwa ysawa na silaha kamili  maangamizi makubwa ya vitani."

 Wakati Bunge la Marekani likionekana kujiandaa kujadili uwezekano wa kudhibiti umiliki wa bunduki kwa mara ya kwanza, imebainika kuwa huenda Paddock alipanga kufanya mashambulizi kama hayo katika miji mingine mikuu.

Mwandishi: John Juma/AFP/RTRE

Mhariri:  Mohammed Abdul-Rahman

 

Albanian Shqip

Amharic አማርኛ

Arabic العربية

Bengali বাংলা

Bosnian B/H/S

Bulgarian Български

Chinese (Simplified) 简

Chinese (Traditional) 繁

Croatian Hrvatski

Dari دری

English English

French Français

German Deutsch

Greek Ελληνικά

Hausa Hausa

Hindi हिन्दी

Indonesian Bahasa Indonesia

Kiswahili Kiswahili

Macedonian Македонски

Pashto پښتو

Persian فارسی

Polish Polski

Portuguese Português para África

Portuguese Português do Brasil

Romanian Română

Russian Русский

Serbian Српски/Srpski

Spanish Español

Turkish Türkçe

Ukrainian Українська

Urdu اردو