1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mjerumani aliemchezea msichana aachiwa

15 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CbxP

ANKARA

Mahkama ya Uturuki imemuachilia mvulana wa Kijerumani mwenye umri wa miaka 17 kutoka gerezani baada ya kuwepo mahabusu kwa miezi minane kwa madai ya kumchezea kingono msichana wa Uingereza mwenye umri miaka 13.

Mawakili wa msichana huyo wanasema mashtaka dhidi yake yanaendelea kubakia.Mahkama imehukumu kwamba Marco Weiss anaweza kurudi nyumbani Ujerumani lakini kesi yake itaendelea hapo mwezi wa April na waendesha mashtaka wanaendelea kusisitiza kwamba ahukumiwe kifungo cha miaka 15 gerezani.

Kijana huyo wa Kijerumani amekanusha kuwa na hatia.