1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkataba wa kusitisha vita Congo watiwa sahihi jumanne

21 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CvZN

KINSHASA:

Serikali ya Jamhri ya Kidemokrasi ya Congo pamoja na makundi ya waasi wanaozozana na pia ya wanamgambo watatia sahihi muafaka hapo kesho jumanne ili kumaliza mapigano ambayo yameathiri upande wa mashariki wa nchi hiyo. Maafisa wa serikali, pamoja na mabalozi wamesema hayo leo.

Mkataba ambao utahusu kusitisha mapigano, umetangazwa kufuatia mazungumzo ya ziadi ya wiki mbili, katika mji wa Goma ambao ndio mji mkuu wa jimbo la Kivu kaskazini linalopatikana mashariki mwa nchi hiyo.Mkutano wa Goma, umewakutanisha pamoja, wajumbe wa serikali,viongozi wa makundi hasimu pamoja na viongozi wa kimkoa.