1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mke wa mgombea urais alipwa euro 600,000

Mohammed Khelef
25 Januari 2017

Mke wa mgombea urais wa Ufaransa anayeongoza, Francois Fillon, anatuhumiwa kupokea euro 600,000 kwa ajira ambayo kamwe hajawahi kuifanyia kazi

https://p.dw.com/p/2WMgt
Penelope Fillon
Picha: picture-alliance/abaca/C. Liewig

Kwa mujibu wa gazeti la dhihaka liitwalo Le Canard Enchaine, Penelope Fillon alikuwa akilipwa fedha hizo kwa kazi ya kuwa msaidizi wa masuala wa kibunge ya mumewe na baadaye kama naibu kwenye bunge la taifa na kisha kwenye kazi katika jarida moja la mambo ya kitamaduni. 

Hata hivyo, gazeti la Le Canard Enchaine linasema hakuna ushahidi ikiwa mwanamke huyo aliwahi kufanya kazi yoyote kati ya hizo ambazo alikuwa akilipwa mishahara. 

Mwenyewe Fillon amesema hivi leo (Jumatano, Januari 25) kwamba amekasirishwa sana na ripoti hiyo ambayo ameiita ya "uchochezi na upotoshaji".

"Nimekasirishwa na uchafuaji huu na uzushi wa makala hii," alisema Fillon, ambaye ni waziri mkuu wa zamani wa Ufaransa akiwa upande wa wahafidhina na ambaye sasa anawasia urais kwa tiketi cha chama Republican kwa uchaguzi utakaofanyika tarehe 23 Aprili na 7 Mei mwaka huu. 

Mwandishi: Mohammed Khelef/Reuters
Mhariri: Josephat Charo