1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkenya aweka rekodi ya olimpik

14 Agosti 2008

Jason Dunford atamnba katika mita 100 kipepeo(butterfly).

https://p.dw.com/p/ExKy

Katika siku ya 6 ya michezo ya olimpik ya Beijing leo,rekodi 6 za olimpik ziliwekwa katika mashindano ya kuogolea na moja na Mkenya Jason Dunford.Muda wake katika mita 100 kipepeo(butterfly) wa sek.51.14 ulikuwa sek.0.09 wa kasi zaidi kuliko ule wa bingwa wa mabingwa- Muamerika Michael Phelps katika michezo ya olimpik ya Athens, Ugiriki 2004. Hii ilikuwa kabla mserbia Cavic kuchukua muda wa sek.51.14 kasi zaidi kuliko mkenya huyo.

Mzimbabwe Kirsty Coventry aliekwishanyakua medali 3 za fedha,amevunja rekodi ya mita 200 kuogolea kimgongo-mgongo (backstroke).muda wake wa rekodi ni dakika 2:06.76.

Katika Orodha ya Medali,Ujerumani sasa ina medali 11,lakini ni sita tu za dhahabu.Wenyeji china wangali wanaongoza kileleni kwa medali 35-ishirini mbili za dhahabu ikifuata Marekani kwa medali 34-huku 10 zikiwa za dhahabu.

Kesho ijumaa majogoo wa Afrika mashariki-Kenya,Ethiopia na hata Tanzania wataanza kuingia uwanjani na medali ya kwanza ya dhahabu itakua katika mita 10.000 wanawake.Je, itaenda Ethiopia au kenya ?