1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkoa wa Nyanza uko tayari kwa uchaguzi

3 Machi 2013

Maandalizi ya upigaji kura katika eneo la nyanza ya kati linalojumuisha kaunti za Kisumu Siaya na Homa Bay yamekamilika.

https://p.dw.com/p/17pOC
A woman carries her baby as she walks past an Orange Democratic Movement (ODM) campaign poster in Kibera slum in capital Nairobi February 27, 2013. Kenya will hold its presidential and parliamentary elections on March 4. REUTERS/Siegfried Modola (KENYA - Tags: ELECTIONS POLITICS)
Kenia Wahlkampagne in Kibera Slum bei NairobiPicha: Reuters

Afisa wa kamati ya kusimamia uchaguzi katika maeneo hayo Bwana Rasi Masudi amesema tayari vifaa vyote vya upigaji kura vimepokelewa na viko chini ya ulinzi mkali tayari kusafirishwa kuenda katika vituo vya kupigia kura hii leo. Kadhalika amekanusha madai kwamba huenda kukawa na tatizo la usambazaji matokeo kwa njia ya dijitali kweye maeneo yasiyo na mtandao mzuri wa mawasiliano ya habari.

Wagombea viti mbali mbali kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika nchini Kenya kesho jumatatu wamekamilisha kampeni zake. Hali imekua hivi hapa mjini Kisumu na nchini kote kwa jumla kwenye kampeni hizi ambazo zilikamilika rasmi saa sita za usiku. Mbali na kuwarai wananchi wawapigie kura, wito mkubwa umekuwa ni kuwaomba wananchi kupiga kura kwa amani na kukubali matokeo yeyote.

Afisa wa kamati ya kusimamia uchaguzi katika eneo la Nyanza ya Kati linalojumuisha mji wa Kisumu Bwana Ras Masudi amewahakikishia wapiga kura wote kuwa maandalizi yote yameishakamilika na kuwa shughuli hii itafanyika vyema kabisa. Ametoa wito warauke ili shughuli ikamilike mapema bila matatizo.

Muungano wa CORD wake mgombea urais Raila Odinga una umaarufu mkubwa mkoani Nyanza
Muungano wa CORD wake mgombea urais Raila Odinga una umaarufu mkubwa mkoani NyanzaPicha: Will Boase/AFP/Getty Images

Anasema, "Tungependa wananchi kujitokeza mapema, vituo vitafunguliwa saa 12 za asubuhi na mbali na kuwa wezesha maafisa wa kura kufanya kazi yao mapema, kuja mapema kutawasaidia watu kutochomwa na jua kali linalowaka hapa na tafadhali ukisha piga kura, rudi nyumbani kwani matokeo yatakua kwenye radio na tv"

Kadhalika amekanusha madai kuwa usambazaji wa habari kwa njia za dijitali huenda ukaadhiriwa na mtandao mbaya wa mawasiliano katika baadhi ya sehemu na kutoa mwanya wa kubadilisha matokeo. Mkuu wa polisi mkoani Joseph Ole Tito amewahakikishia pia usalama wakazi wa hapa….anasema "Kuanzia sasa mtawaona askari wengi sana wakishikadoria, tuna ndege ya helicopter pia, tungependa kuwaomba wananchi kutokuwa na wasiwasi wanapowaona kwani wako hapa kuwalinda ili muweze kupiga kura na kuendelea vyema na shuhuli zenu"

Mji wa Kisumu na mkoa wa nyanza kwa jumla ndio ngome kubwa ya mgombea urais kwa muungano mkubwa wa kisiasa wa cord Raila Odinga na wapiga kura hapa wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi. Kwenye kampeni yake ya mwisho hapa siku ya ijumaa, Raila aliomba wapiga kura kuruka na adhana ya waislamu ya fajri ili kupiga kura mapema. vilabu vyote vya pombe na imeamriwa kufungwa hapa kuanzia leo hadi jumanne.

Mwandishi: John Marwa, DW Correspondent Kisumu
Mhariri: Sekione Kitojo