1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano kati ya Afrika na Ulaya

9 Desemba 2007

---

https://p.dw.com/p/CZPv

LISBON:

Taarifa kutoka Lisbon zasema mkutano wa pili kati ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa nchi za kiafrika umeidhinisha hii leo mpango wa kujenga uhusiano wa pande mbili zilizo sawa baina ya mabara haya 2.Viongozi hao wakitazamiwa kumaliza mkutano wao leo kwa kuafikiana juu ya mkakati wa ushirikiano kwenye maswali ya uhamiaji,biashara,nishati,mabadiliko ya hali ya hewa n a maendeleo.Isitoshe, UU unapanga kuvipa vikosi vya kuhifadhi amani barani Afrika msaada zaidi wa fedha.

Nchi za kiafrika kwa upande wao nazo, zinatakiwa kuchukua jukumu la kuheshimu haki za binadamu.

Taarifa kandoni mwa duru za mkutano mjini Lisbon, zasema pande hizo mbili zimeshindwa kuelewana juu ya mapatano mapya ya biashara kati ya mabara yao 2. Rais Abdoulaye Wade wa Senegal,amesema sehemu kubwa ya viongozi wa Afrika wanapinga mapendkezo ya UU ya biashara huru-EPA.

Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani,

alimlaumu rais Mugabe wa Zimbabwe, kuharibu jina la bara la Afrika kwa kukanyaga nchini mwake haki za binadamu. Alisema,

„Wakati unapita na hali za wananchi zazidi kuwa mbaya.

Labda huu ni mchango mdogo tu ikiwa mabadiliko huko yatatokea haraka.“

Jumuiya ya SADC ya ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo kusini mwa Afrika imeutuhumu Umoja wa Ulaya kuuingiza mzozo wa Zimbabwe katika ajenda ya mkutano huu wa Lisbon.SADC inadai ,mada ya Zimbabwe haikuwamo katika ajenda iliokubaliwa na pande mbili.

Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown, ameususia mkutano wa Lisbon kutokana na kuhudhuria kwa rais Mugabe.

Kuhusu ushirikiano kati ya UA na UU rais wa Ghana John Koufour alisema:

„Afrika inaihitaji Ulaya sawa na Ulaya inavyoihitaji Afrika.“

LISBON

Katibu mkuu wa zamani wa UM Kofi Annan, ameitisha „mapinduzi ya kilimo“ barani Afrika yakiiingiza ushirika baina ya serikali za Afrika na wakulima ili kuondosha njaa katika bara hili masikini.Annan alisema hayo kandoni mwa mkutano wa kilele wa Afrika na Ulaya mjini Lisbon jana.

Hapo kabla, waziri mkuu wa Spain Jose Luis Zapatero, alipendekeza mkataba kati ya UA na UU kupambana na uhamiaji usio halali.Zapatero alisema mapatano ya aina hiyo yalenge kukuza elimu,nafasi za kazi na kujenga miundo mbinu katika nchi zenyewe .