1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano kuhusu amani waanza leo mjini Goma

6 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Ckvw

Mkutano wa siku nane kuhusu amani katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, unaanza rasmi hii leo katika mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, Goma.

Mwenyekiti wa kamati iliyouandaa mkutano huo padre Appollinaire Malu Malu, amesema sherehe za ufunguzi wa mkutano huo zitafanyika katika uwanja wa chuo kikuu huru cha maziwa makuu mjini Goma.

Ukiwa umeandaliwa kufuatia juhudi za rais Joseph Kabila, mkutano huo unalenga kumaliza mizozo kati ya mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, inayopakana na Rwanda na Burundi, na kujenga misingi ya amani ya kudumu mashariki mwa Kongo.

Mkutano huo umewahi kuahirishwa mara moja na kuna wasiwasi ikiwa kiongozi wa waasi, jenerali muasi Laurent Nkunda, atahudhuria.