1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano kuhusu kuwarejesha makwao wakimbizi wafanyika Goma

Josephat Nyiro Charo27 Julai 2010

Mkutano huo umewaleta pamoja wajumbe kutoka Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR

https://p.dw.com/p/OW2k
Maelfu ya wakimbizi wakirudi kwao kaskazini mwa GomaPicha: AP

Mkutano unaolenga kupanga mikakati ya kuwarudisha nyumbani wakimbizi kutoka Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, unafanyika mjini Goma mashariki mwa nchi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mkutano huo umewakusanya pamoja wajumbe kutoka Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia wakimbizi, UNHCR. Mkutano huo unafuatia ule uliofanyika mjini Kigali, Rwanda, mwezi Februari mwaka huu.

Mwandishi wetu aliyeko Goma, John Kanyunyu ametutumia ripoti ifuatayo.

Mwandishi: John Kanyunyu

Mhariri: Josephat Charo