1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano mkuu wa chama cha CDU na kura ya maoni Venezuela

Oummilkheir4 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CWbf

Mkutano mkuu wa chama cha Christian Democratic Union –CDU na kushindwa kura ya maoni ya katiba nchini Venezuela ndio mada zilizowashughulisha zaidi wahariri wa Ujerumani hii leo.Hata hivyo kuna baadhi ya magazeti yaliyoendelea kuchambua uchaguzi wa bunge nchini Urusi.

Tuelekee kwanza lakini Hannover ambako gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG linamulika hotuba ya kansela Angela Merkel na kuandika:

“Merkel hakuonyesha shangwe wala kivutio.”Mrengo wa kati” kauli mbiu ya mkutano huo mkuu,ndio matamshi mtu aliyoweza kuyasoma nyuma yake.CDU inataka kumshughulikia takriban kila mtu.Mrengo wa kati ni uwanja mpana.Ndio maana siasa ya mrengo wa kati inatafsirika pia kama mkondo huu na ule.Na ndio maana hotuba ya Merkel ilikua kama ujumbe unaosema”hiki lazma ufanye na kile ,pia usikiwache.Siasa ya mrengo wa kati inatakiwa iwe ya kutegemea.Mkondo ule ule ,hakuna kutanga tanga ,huo ndio ujumbe wa Angela Merkel.Siasa kama hiyo lakini haizushi tamaa kubwa,hata haiawasumbui watu muda mfupi kabla ya uchaguzi.Siasa kama hiyo ni chapwa , badala ya watu kujiandaaa wanajikuta wakiongoza.

Gazeti la KÖLNER STADT ANZEIGER linahisi:

Merkel ameshadidia na kusisitiza umuhimu wa kufuata mkondo mpya.Hakushangiriwa sana lakini.Na kama kuna walioshangiria basi ni pale tuu SPD waliposhambuliwa.Kinyume chake ni shida kuelezea au kufafanua japo kidogo mkondo wa chama.Muongozo mpya wa chama kwa kweli hausaidii pakubwa.Kila mtu anazingatiwa.Lakini hali kama hiyo inawezekana tuu kama mpinzani wa kisiasa ni dhaifu na kama ukuaji wa kiuchumi unajaza makasha bila ya shida.

Mada ya pili magazetini ni kuhusu kushindwa kura ya maoni ya wananchi nchini Venezuela.Gazeti la FRANKFURTER RUNDSCHAU linaandika:

Naiwe haba vipi- rais Chavez alikwishawahi kondolewa patupu katika vituo vya upigaji kura kwa mara ya mwanza mnamo mwaka 1999.Waliosababisha ashindwe sio wapinzani wake,hasha,wafuasi wake mwenyewe.

Kwa maneno mengine, ni wale wanaohisi kua Chavez ni kiongozi mzuri,hawapingi hata kidogo namna anavyojitokeza hadharani, hawaudhiki na mfumo wake usio bayana wa ujamaa kwa karne ya 21 ,wala juhudi zake za kuinua hali ya jamii-lakini wameingiwa na hofu linapohusika suala la kuguswa katiba.Si hasha mtu akishtuka anaposikia kile rais na wenzake wanachokiwazia.Achaguliwe milele Chavez kua rais,aitawale Venezuela hadi kufikia mwaka 2050!Na sheria ya hali ya hatari !Ajitenge na mfumo wa shirikisho!Awe na madaraka makubwa hata mbele ya matajiri wenye kumiliki mafu.Ahaa,si bure kuwaona hata wana Chavista wanaingiwa na hofu.!

Kwa maoni ya NEUE OSNABRÜCKER ZEITUNG,matumaini ya kuendelezwa demokrasi hayakutoweka nchini Venezuela.Gazeti linaendelea kuandika:

„Alitaka kuyazima kabisa.Lakini hesabu zake zimeshindwa.Kuna hatari kidogo ndani yake,sawa na fursa ambao si ndogo.Cha kuhofiwa zaidi ingekua kama wafuasi wa Chavez wangefanya fujo.Au wangetanabahi na kutambua mwanya kati ya serikali na upande wa upinzani lazma uondolewe na masilahi ya taifa kutangulizwa mbele.