1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano Mkuu wa Chama cha CDU

Abdu Said Mtullya5 Desemba 2012

Chama Kikuu katika serikali ya mseto ya Ujerumani CDU kimepitisha pensheni zaidi kwa akina mama wazazi, kwenye mkutano wake mkuu mjini Hannover, kaskazini mwa Ujerumani.

https://p.dw.com/p/16wCm
Mwenyekiti wa chama cha CDU Angela Merkel
Mwenyekiti wa chama cha CDU Angela MerkelPicha: picture-alliance/dpa

Lakini wajumbe hawakukubaliana juu ya kuwapa haki sawa za kodi , watu wanaoishi katika ndoa za jinsia sawa. Wajumbe zaidi ya alfu moja wamepitisha maamuzi kadhaa wenye mkutano wao mkuu juu ya pensheni na kuhimiza idadi maalumu ya wanawake katika sehemu za uongozi. Chama cha CDU pia kimeahidi kuendelea kuweka milango wazi kwa ajili ya wahamiaji.

Akiwahutubia wajumbe katika juhudi za kuwahamasisha juu ya kampeni za uchaguzi mkuu utakayofanyika mwaka ujao, Mwenyekiti wa CDU bibi Angela Merkel ambae pia ni Kansela wa Ujerumani amesema chama cha CDU kimeyazingatia masuala muhimu. "Tumeweka msingi wa programu ya uchaguzi.Tunapasa kuangaza mbele." Bibi Merkel amesema sasa imebakia miezi kumi ya kuitayarisha programu ya uchaguzi mkuu pamoja na washirika wa Christian Democratic Union." Kansela Merkel amewataka wanachama wa CDU waitafakari Ujerumani ya mafanikio ya kati ya mwaka wa 2013 na 2017.

Bibi Merkel aliechaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa chama cha CDU kwa mara ya saba amewataka wanachama wa chama chake wauangalie mustakabal kwa kuizingatia hali halisi kwamba wananchi ndiyo muhimu na hivyo inapasa kuenda kwa wananchi hao.Bibi Merkel amesema kampeni za uchaguzi zimebadilika. Inapasa kuenda kwa watu hao. Haitoshi kutayarisha ilani ya uchaguzi au kuwatumia wapiga kura programu ya uchaguzi."

Delegates sing the national anthem at the end of a congress of Germany's ruling conservative Christian Democratic Union (CDU) party on December 5, 2012 in Hanover, central Germany. Chancellor Angela Merkel was overwhelmingly re-elected her party's leader on December 4 as she kicked off her bid for a third term, saying only she could steer Germany through turbulence at home and abroad. AFP HOTO / JOHN MACDOUGALL (Photo credit should read JOHN MACDOUGALL/AFP/Getty Images)
Wajumbe wa mkutano wa CDUPicha: John MacDougallAFP/Getty Images

Kwenye mkutano wao mkuu wa siku mbili,wajumbe wa chama cha CDU pia walipiga kura kwa idadi kubwa kuunga mkono hatua ya kupiga marufuku kinachoitwa msaada wa kuwawezesha watu kujiua wenyewe.

Hapo awali viongozi muhimu ikiwa pamoja na aliekuwa kiongozi wa wabunge wa CDU bungeni, Volker Kauder na Mwenyekiti wa chama ndugu cha CSU Bwana Horst Seehofer walisisitiza umuhimu wa mfungamano na chama cha Waliberali lakini wamepinga kuunda mseto na chama cha kijani.

Hata hivyo kwa mujibu wa wachambuzi huenda mfungamano wa vyama vya kihafidhina ukakabiliwa na ugumu katika uchaguzi mkuu ujao kutokana na mshirika wao- chama cha kiliberali kulega nyuma katika kura za maoni. Kwa mujibu wa wachambuzi chama cha waliberali FDP huenda kikashindwa kuruka kiunzi cha asilimia tano ili kuweza kuingia bungeni.

Juu ya mkutano mkuu wa chama cha CDU kwa jumla mchambuzi mmoja amesema siku mbili za majadiliano zimethibitisha mafanikio ya Mwenyekiti Angela Merkel zaidi kuliko ya chama kwa jumla.

Mwandishi: Mtullya Abdu/dpa

Mhariri: Mohammed Khelef