1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano mkuu wa SPD na Mazishi ya Helmut Kohl magazetini

Oumilkheir Hamidou
26 Juni 2017

Mkutano mkuu wa chama cha Social Democratic SPD, mjini Dortmund na kivuli katika mazishi ya kansela wa muungano Helmut Kohl ndio mada mbili kuu zilizohodhi magazetini

https://p.dw.com/p/2fNtQ
Deutschland SPD-Bundesparteitag
Picha: Reuters/W. Rattay

 

Tunaanzia Dortmund ambako jana viongozi wa chama cha Social Democratic-SPD wamepitisha  kwa sauti moja waraka wa sera wanazozipigania kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwezi Septemba mwaka huu. Maoni ya wahariri yanalingana, hawaamini kama waraka huo utasaidia kupindua wezani wa nguvu bungeni. Gazeti la "Landeszeitung" linaandika. "Sera zinazopiganiwa na SPD zimeshatangazwa. Zinatoa picha ya msimamo halisi wa wana Social Democrat sawa na zinavyoonyesha kuwa kivutio kwa ajili ya mazungumzo ya kuunda serikali ya muungano pamoja na vyama vya FDP, walinzi wa mazingira die Grüne, vyama ndugu vya CDU/CSU na pia wafuasi wa siasa kali za mrego wa kushoto die Linke. Na kwa kumteuwa Martin Schulz, SPD wamempata kiongozi anayeweza pia kushambulia. Lakini mashambulio yake dhidi ya kansela yamekithiri. Kuzungumzia juu ya hujuma dhidi ya demokrasia ni hatari na kosa pia. Kinachokosekana ndani ya chama cha SPD ni kiu cha mageuzi. Kama ilivyokuwa mwaka 1998 pale wananchi walipokuwa na kiu cha mageuzi baada ya miaka 16 ya utawala wa Helmut Kohl, kwasababu ya mkwamo wa kisiasa na umuhimu wa mageuzi. Lakini kiu cha mageuzi kitokee wapi mwaka 2017, ikiwa idadi ya wasiokuwa na kazi inaazidi kupungua na makasha ya haina ya taifa yamesheheni? Kwa maneno mengine: wananchi wanakinai na imani yao kwa kansela Merkel ni kubwa kuputa kiasi."!

 

Gazeti la "Schwäbische Zeitung" linajiuliza sababu zilizopelekea chama cha SPD kupungukiwa na imani ya wapiga kura baada ya imani hiyo kuongezeka Martin Schulz alipoteuliwa kugombea kiti cha kansela. "Hotuba kali si chanzo cha mageuzi. Kwa nini SPD wameporomoka tena baada ya imani ya wapiga kura kupanda baada ya Martin Schulz kuchaguliwa kugombea kiti cha kansela, suala hilo si rahisi kulijibu. Na jibu pia halitokani na majukumu ya SPD na CDU/CSU. SPD wanafanya bidii, wanachapisha waraka wa sera zao  ikiwa ni pamoja na kodi za mapato na malipo ya uzeeni-sera zote zinastahiki sifa. Martin Schulz anachochea mjadala na wanapania kuongoza. CDU/CSU hawasemi chochote, na kansela Merkel anautumia ule usemi: si mnanijua! Lakini pengine sababu si Merkel, lakini ni Erdogan,Trump na Putin na ndio maana wajerumani wanahisi haweahitaji kuwa na hofu Merkel akiendelea kuwa kansela.

Mfarakano kati ya mjane wa Helmut Kohl na taasisi za serikali na wanawe

Mada ya pili magazetini inahusiana na kivuli kilichotanda katika maandalizi ya mazishi ya kansela wa muungano, muasisi mmojawapo wa Umoja wa ulaya Helmut Kohl. Gazeti la Märkische Oderzeitung linaandika: "Matamshi wa Walter Kohl, mtoto mkubwa wa kiume wa kansela wa zamani, kwamba hatoshiriki katika mazishi ya babaake yakifanyika Speyer, ni ushahidi  bayana wa mzozo mkubwa ulioko. Bila ya kuitaja picha iliyokuwemo magazetini na kumuonyesha jinsi alivyozuwiliwa  pamoja na wanawe kuingia ndani ya nyumba ya wazee huko Oggersheim.

 

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri:Josephat Charo