1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa amani,usalama na maendeleo wafunguliwa Goma

Oummilkheir6 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cl1T

Mkutano wa amani kwa majimbo ya kaskazini na kusini ya Kivu-katika eneo la mashariki la jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo unaanza hii leo mjini Goma.Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya kamati ya maandalizi ya mkutano huo.Katika mkutano pamoja na waandishi habari,mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo Askofu Appolinaire Malu Malu amesema sherehe za ufunguzi za mkutano wa amani,usalama na maendeleo katika eneo la kaskazini na kusini mwa Kivu zitafanyika leo katika ukumbi wa “chuo kikuu huru cha maziwa makuu” mjini Goma.Mkutano huo unaitishwa kutokana na juhudi za rais Joseph Kabila na umelengwa kumaliza mivutano katika maeneo yanayopakana na Burundi na Rwanda pamoja na kuleta amani ya kuudumu katika maeneo hayo.