1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa chama cha ANC cha Afrika Kusini

28 Juni 2007

Chama tawala cha African National Congress, ANC, cha Afrika Kusini kimeanza leo kuwa na mkutano wake mkuu, huku rais wa nchi hiyo,Thabo Mbeki, akikiri kwamba mabalaa mawili ya umasikini na ukosefu wa nafasi za kazi bado hayajapatiwa dawa nchini humo, licha ya kwamba mafanikio mengi yamepatikana tangu chama hicho kuweko madarakani na kuporomoka mfumo wa ubaguzi wa rangi mwaka 1994.

https://p.dw.com/p/CHBz
Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini
Rais Thabo Mbeki wa Afrika KusiniPicha: AP

Pia alikiri kwamba haiwezekani kuyatanzua matatizo ambayo yamelimbikizwa mnamo miaka 350 kwa miaka 13 tu ya demokrasia.

Zaidi kutoka kwa Max Bushoke akiwa Johannesburg.