1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Commonwealth utamalizika leo

25 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CSuK

Kampala:

Viongozi wa jumuia ya madola, Commonwealth wanaokutana mjini Kampala Uganda,wameyataja mabadiliko ya hali ya hewa kua ni kitisho kwa baadhi ya visiwa vidogo vidogo- wanachama wa jumuia hiyo .Hata hivyo jumuia ya Commonwealth haijatangaza hatua zozote zinazowalazimisha wanachama wake wapunguze moshi wa sumu unaotoka viwandani.

Taaarifa iliyotangazwa Kampala mnamo siku ya pili ya mkutano wa kilele wa jumuia ya Commonwealth,imesema halai ya kutofanya chochote itagharimu zaidi kuliko kupitishwa haraka hatua za kuepusha kutzidi hali ya ujoto duniani.Mkutano wa kilele wa jumuia ya madola Commonwealth unatarajiwa kumalizika hii leo mjini Kampala nchini Uganda.