1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa dharura waidhinisha mkopo kwa Ugiriki

8 Mei 2010

Viongozi wa mataifa 16 yanayotumia sarafu ya Euro, wameidhinisha mkopo wa kuikoa Ugiriki ili isije ikafilisika. Uamuzi huo umepitishwa katika mkutano wa dharura mjini Brussels,Ubeligiji.

https://p.dw.com/p/NJFK
German Chancellor Angela Merkel arrives for an EU summit at the EU Council building in Brussels, Friday, May 7, 2010. The 16 leaders of the euro zone meet Friday to finalize the Greek rescue plan and assess how such financial crises can be avoided in the future. (AP Photo/Geert Vanden Wijngaert)
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel.Picha: AP

Wakati huo huo, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alisema kundi hilo la mataifa 16, litatoa ujumbe maalum kwa walunguzi, kwa kuanzishwa mfuko maalum wa dharura, kwa azma ya kuzuia matatizo ya deni katika mataifa mengine ya Ulaya.

Serikali ya Ugiriki imechukua jukumu la kubana matumizi yake katika jitahada za kufanya mageuzi makubwa ya kiuchumi ili nchi hiyo iweze kupata mikopo ya dharura kutoka nchi za kanda ya euro na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF.

Greek Prime Minister George Papandreou speaks during a debate in Parliament on the country's planned new austerity measures on Thursday, May 6, 2010. Papandreou said Greece's only hope of avoiding bankruptcy is to approve the measures to secure money from a joint EU and International Monetary Fund rescue package. He spoke during a heated debate overshadowed by the deaths of three people during protests against spending cuts. The 300-member house, in which the governing Socialists hold a strong majority, was due to approve the law later Thursday. (AP Photo/Petros Giannakouris
Waziri Mkuu wa Ugiriki, George Papandreou.Picha: AP

Hatua hiyo ya serikali ya Ugiriki imepingwa vikali na raia nchini humo. Waziri Mkuu wa Ugiriki George Papandreou alipozungumza mjini Brussels alisema sio nchi yake pekee inayokabiliwa na matatizo ya deni.

Nchini Ujerumani, wabunge mjini Berlin, wameidhinisha mswada wa sheria inayofungua njia ya kuipatia mkopo Ugiriki. Rais wa Ujerumani, Horst Köhler ametia saini mswada huo kuwa sheria.

Kuambatana na makubaliano ya mkopo huo, Ujerumani itaipatia Ugiriki Euro bilioni 22. Ujerumani inatoa sehemu kubwa ya mkopo unaotolewa na nchi zinazotumia sarafu ya Euro, kwa sababu pia ni nchi iliyo na uchumi mkubwa kabisa katika kundi la mataifa 16 yanayotumia Euro.

Mwandishi: Munira Muhammad/AFPE

Mhariri:P.Martin