1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Doha

Oumilkher Hamidou30 Novemba 2008

Duru ya mazungumzo ya Doha kufufuliwa kabla ya X-Mas

https://p.dw.com/p/G6Ci

Doha:

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon ameyahimiza mataifa tajiri kiviwanda yasiachie juhudi za kupambana na ugaidi kua chanzo cha kupuuza vita dhidi ya umaskini.Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban-Ki-Moon amesema hayo mbele ya wajumbe wanaohudhuria mkutano wa kimataifa kuhusu maendeleo.Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa na rais Mahmoud Ahmadinedjad wa Iran ni miongoni mwa viongozi wa kimataifa wanaohudhuria mkutano huo wa Doha utakaomalizika jumanne ijayo.Sheikh Hamad bin Khalifa al-Thani wa Qatar,mwenyekiti mwenza wa mkutano huo amesema si haki kutaraji mataifa tajiri kwa mafuta yawajibike zaidi katika vita dhidi ya umaskini.Wakati huo huo kiongozi wa shirika la biashara la kimataifa WTO anasema wakati umewadia wa kufufua duru ya mazungumzo ya Doha kuhusu biashara huru.Pascal Lamy amesema anafikiria kuitisha mkutano mjini Geneva mapema mwezi ujao,kwa sharti lakini kama makubaliano yatafikiwa.Baadhi ya viongozi wa dunia wanahisi sheria huru za kibiashara zinaweza kusaidia kuukwamua uchumi unaolega lega wa dunia.Mazungumzo ya Doha yamelengwa kupunguza vizuwizi vya kibiashara na kuhakikisha biashara ya haki kwa nchi zinazoinukia.Ruzuku wanazolipwa wakulima,hasa barani Ulaya na nchini Marekani ndio mzizi wa fitina katika mazungumzo hayo yaliyoanzishwa katika mji mkuu wa Qatar-Doha ,miaka sabaa iliyopita.