1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa G-8-kandoni

7 Juni 2007

Kandoni mwa mkutano wa nchi tajiri za kiviwanda G-8 huko Heiligendam,mashariki mwa Ujerumani,vikundi vya wakereketwa vinaandamana,Vilio vinasikika kuzuwia uchafuzi wa hali ya hewa na kuzisaidia nchi masikini hasa za Afrika.

https://p.dw.com/p/CHke
Rais Bush na mwenyeji wake Angela Merkel(G-8)
Rais Bush na mwenyeji wake Angela Merkel(G-8)Picha: AP

Nje ya ukumbi wa viongozi wa dola kuu 8 za kiviwanda ulimwenguni-G-8 huko Heilingendam,vikundi mbali mbali vya wakereketwa vimeaanda navyo mikutano yao:vinapigania ulimwengu wa haki,vinapinga vita na unyonyaji, uchafuzi wa mazingira,umasikini na janga linalozidi kuenea la maradhi ya ukimwi.

Karibu na kituo cha mkutano wa kilele wa G-8, kiasi cha wapinzani 3000 wa mkutano huo wamekusanyika nje ya uwa wa senyenge –mpaka unaowakinga na viongozi wanaokutana – polisi imearifu.Kwa sasa, hali imetulia baada ya machafuko yaliozuka wakati wa changamoto kati ya wakereketwa wanaoupinga utandawazi na vikosi vya polisi.

Kwani, jana polisi walitumia mabomba ya maji kuwatimua hadi waandamanaji 10.000 waliojaribu kunyemelea ukumbi wa mkutano.

Mbali na waandamanaji kuna vikundi vinavyoelewa uzuri kabisa maafa ya shida,madhila na udhalimu upitao katika dunia hii.Miongoni mwao ni muafrika Kusini Mavasa Nkheseni,mkereketwa wa vita dhidi ya ukimwi.

Nkhesani amevaa shati la rangi ya manjano likiwa na maandishi “NINA UGUA UKIMWI”.(HIV POSITIV).

Mavasa asema:

“Nilikua katika hali kama hii:Sijahitaji kukhadithia,ilibidi nifunge mdomo kwa sababu ni kwa muujibu wa mila zetu ni aibu watu wengine kujua juu ya maradhi kama haya.Nikabidi kunyamaa kimya kutoelezea hali yangu,hisia zangu na maovu yote yalionipata.”

Mwanzoni mwa mkutano mkuu wa kanisa la kiinjili mjini Cologne,mbali sana na Rostock,mashariki mwa Ujerumani unakoendelea wakati huu mkutano wa G-8,mkutano wa kilele wa kundi la dini 8 mbali mbali ulidai hatua madhubuti zichukuliwe ili kupiga vita maafa mengine-njaa.

Katika taarifa na mwito wake mkutano huo wa kilele wa dini 8 kuu 8 ulimwenguni, umeeleza “ufukara mkubwa ulioenea katika dunia yetu ni aibu na kshfa kubwa.” Wolfgang Huber alisema:

“Sasa wakati umewadia kuondosha umasikini.Hii ni risala inayotoka Cologne kwenda Heilingendam”-

Leo kutafanyika pia burdani kubwa ya muziki ikijumuisha vigogo kama Bono,Bob Gelsdorf na mjerumani Herbert Grönemeier kuhamasisha viongozi wanaokutana wa G-8 kutimiza ahadi zao walizotoa huko Gleanageles,Scotland kwa nchi masikini.

Bono amekuwa akidai tangu kuwasili Ujerumani na hata kabla, kushindwa kutimiza ahadi ulizotoa kwa masikini ni aibu.

“Tunataka kutimizwe ahadi za millennium zilizotolewa na nchi zote tajiri za kiviwanda pamoja na kupunguzwa kwa nusu umasikini hadi ifikapo mwaka 2015.Hii yawezekana.”

Mada nyengine inayozusha hamasa kubwa mkutanoni na nje yake ni jinsi gain kuzuwia kuchafuka zaidi kwa hali ya hewa.Taarifa zilizoufikia mkutano huu wa G-8 huko Heiligendam,zasema India kupunguzas moshi wake unaochafua mazingira.

Ikiwa ni mchafuzu 5 mkubwa duniani na m ojawapo ya mataifa yanayokua kwa nguvu kiuchumi wakati huu kama china, India imejikuta ikishinikizwa sana tangu na Umoja wa Ulaya na Marekani kupunguza moshi wake unaopaa hewani kutoka viwanda vyake.Waziri-mkuu wa India Manmoham Singh anahudhuria pia mkutano huu wa kundi la G-8,huko Heiligendamm.