1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa G20 wazungumzia ukwepaji wa kodi

17 Machi 2017

Mji wa Baden-Baden nchi Ujerumani ni mwenyeji wa mkutano wa G20, kundi la nchi zinazostawi kiuchumi ulianza leo.Harakati za maandalizi ya kukaribisha watunga sera za kiuuchumi kutoka nchi mbalimbali duniani zimenza.

https://p.dw.com/p/2ZQkC
Deutschland Vorbereitungen zum G20 Treffen in Baden-Baden
Picha: picture-alliance/dpa/U. Deck

Kwa wale washabiki wa kamari  za  mikahawa ya Casino mjini humo itabidi wasubiri kwa sababu maeneo ya starehe hiyo yatakuwa yamefungwa mpaka Jumamosi jioni.

Sababu ya kufungwa sehemu hizo ni kuwepo kwa mkusanyiko wa viongozi mbalimbali kama vile mawaziri wa fedha,wakuu wa benki kuu wa nchi ishiri zenye nguvu ya kiuchumi duniani.

Ujerumani kwa sasa inashikilia Urais wa kundi hilo la G20, linalowashirikisha nchi 20 muhimu zinazokuwa kiuchumi. Mkutano huo mjini Baden-Baden  ni hatua pia , ya kujianda  kwa ajili ya mkutano wa  kilele wa viongozi unaotarajiwa kufanyika mapema Julai mjini Hamburg.

Waziri wa fedha wa Ujerumani Wolfgang Schäuble anatarajiwa kupambana na maswala ya ukwepaji wa kulipa  kodi wa  makampuni ya kimataifa. Pia sauti yake itasikika katika masuala ya utulivu wa kifedha kupunguza madeni na kutengeneza ushirikiano mpya na Afrika. Kukabilianan na yote hayo, kunahitaji ushirikiano wa kimataifa na ufahamu mzuri juu ya sababu na athari ya vitendo ya kila nchi juu ya nyengine. Lakini kwa upande wa Marekani na sera ya Rais Donald Trump ya " Marekani Kwanza " suala la ushirikiano wa kimataifa  kwa sasa linaonekana kuwa gumu.

Kombobild Merkel Trump 2016 (picture alliance )
Kansela Angela Merkel na rais wa Marekani Donald Trump

Kwa umbande wa Africa kundi hilo la G20 limeelekeza katika mchakato wa kuhakikisha kuwa mpango wa kutengeneza  sera za kimataifa unakwenda bila ya matatizo.

Mradi wa  waziri wa fedha wa Ujerumani Wolfgang Schäuble unaoitwa "Compact with Africa"  unaolenga katika  uwekezaji, kwa  lengo la kutengeneza mazingira bora kwa uwekezaji binafsi katika nchi za Afrika.

Macho yote Washington

Lakini macho yote yako Washington, mbapo kun  masuala ya mabishano kama vile ya kupambana na shughuli za benki kinyume cha sheria, ukwepaji wa kodi wa kimataifa, fedha haramu na ufadhili wa ugaidi. Masuala ambayo yatakuwa katika meza ya majadiliano siku ya Jumamosi.

Kombobild Merkel Trump 2016 (picture alliance )
Kansela Angela Merkel na rais wa Marekani Donald Trump

Washiriki katika mkutano wa G20 mjini Baden-Baden ulioanza leo watalenga  mtazamo wao mjini Washington, ambako huko Kansela wa Ujarumani Angela Merkel anajianda na mazungumzo yake na rais wa Marekani  Donald Trump, katika ikulu ya White House. Bila ya shaka mkutano huo wa viongozi hao wawili huko unaweza kuwa na ushawishi katika majadiliano kwa  mkutano wa G20  mjini Baden-Baden.

Mwandishi : Najma Said

Mhariri  :     Mohammed Abdul-Rahman