1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa G8 waanza

19 Mei 2012

Rais Barack Obama ameufungua rasmi mkutano wa mataifa yenye utajiri mkubwa wa viwanda G8 na kuungana na rais mpya wa Ufaransa kwa kuhimiza kwanza ukuaji wa uchumi badala ya kubana matumizi.

https://p.dw.com/p/14yaT
U.S. President Barack Obama greets Germany's Chancellor Angela Merkel as she arrives at the G8 Summit at Camp David (eingestellt von: qu)
Merkel Obama G8 Camp DavidPicha: Reuters

Rais Barack Obama na viongozi wa mataifa mengine yenye utajiri mkubwa wa viwanda wameweka kando majadiliano juu ya matatizo ya kiuchumi ya mataifa ya Ulaya na Afghanistan hali ambayo itatamalaki mazungumzo ya mkutano huo wa wiki nzima na kuangalia njia za kuimarisha nguvu za mataifa ya dunia dhidi ya maendeleo kuhusu silaha za kinuklia za Iran na kuhimiza jibu la nguvu zaidi katika hali ya ghasia inayozidi kuporomoka nchini Syria.

U.S. President Barack Obama (R) listens as French President Francois Hollande speaks following their bilateral meeting in the Oval Office of the White House in Washington May 18, 2012. Hollande is in the United States to join other leaders of the major industrial economies and meet for a G8 Summit at Camp David this weekend to try to head off a full-blown financial crisis in Europe. REUTERS//Eric Feferberg/Pool(UNITED STATES - Tags: POLITICS BUSINESS)
Barack Obama na Francois HollandePicha: REUTERS

Obama atataka kusikilizwa na wahusika wakuu katika masuala yote katika mikutano ya G8 na jumuiya ya NATO. Majadiliano yatalengwa moja kwa moja au kwa kiasi fulani dhidi ya Urusi, ambayo inaonekana kuwa inazikingia kifua Iran na Syria na mkwamishaji mkubwa wa malengo ya Marekani kama vikwazo vya silaha dhidi ya Syria.

Madeni ya Ulaya

Mkusanyiko huo wa viongozi unakuja katika kivuli cha mzozo wa madeni wa mataifa ya eneo la euro na kuporomoka kwa uungwaji mkono wa umma katika vita vya Afghanistan. Mtafaruku wa kisiasa na kiuchumi nchini Ugiriki na Hispania unaelezea jinsi vipi uchumi wa mataifa ya Ulaya ulivyo tete baada ya kuzipiga chini serikali zinazoshabikia ubanaji wa matumizi.

Waziri wa fedha wa Ujerumani ametabiri siku ya Ijumaa kuwa mzozo huo unaweza kuwepo kwa muda wa miaka miwili mingine.

Bundesfinanzminister Wolfgang Schäuble spricht am Donnerstag (17.05.2012) in Aachen nach der Verleihung des Karlspreises. Mit dem Internationalen Karlspreis zeichnet die Stadt Aachen jedes Jahr Persönlichkeiten aus, die sich besonders um Europa verdient gemacht haben. Foto: Oliver Berg dpa/lnw
Waziri wa fedha wa Ujerumani Wolfgang SchäublePicha: picture-alliance/dpa

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel atakabiliwa na msukumo kutoka kwa Obama na rais mpya wa Ufaransa Francois Hollande kuchukua hatua zaidi zenye lengo la kuchochea ukuaji wa uchumi. Merkel amekuwa akihimiza nchi kupunguza matumizi katika bajeti zao ili kuzuwia kuongezeka kwa madeni. Lakini upunguzaji wa kiwango kikubwa katika matumizi ya serikali umezuwia ukuaji wa uchumi katika mataifa 17 wanachama wa umoja wa sarafu ya euro.

Marekani yategemea Ulaya imara

Kampeni ya Obama kutaka kuchaguliwa tena kuwa rais wa Marekani inaweza kuingia katika utata iwapo bara la Ulaya litatumbukia katika mdororo wa kiuchumi, ikiwa ni mshirika mkuu wa kiuchumi wa Marekani , ama kutumbukia katika mtafaruku wa kifedha iwapo Ugiriki ambayo inakabiliwa ma madeni makubwa ikifikia kujitoa katika umoja wa sarafu ya euro.

Viongozi wa dunia wameungana kwa pamoja na kutoa kauli ya kuunga mkono zaidi msukumo kuelekea sera za kuukuza uchumi ili kupunguza mzozo wa madeni wa mataifa ya Ulaya, ambao unatishia kuiondoa Ugiriki katika kanda ya euro na kusambaa pia katika mataifa mengine pamoja na uchumi wa dunia kwa jumla.

Mwandishi : Sekione Kitojo /rtre/ape

Mhariri : Sudi Mnette