1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa homa ya ndege wafunguliwa Mali

6 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCly

Mkutano wa kimataifa unaojadilia homa ya ndege umefunguliwa rasmi mjini Bamako nchini Mali.Mkutano huo wa siku tatu ni wa nne kufanyika tangu mwisho wa mwaka uliopita.

Kikao hicho kinafanyika barani Afrika kwa mara ya kwanza kwasababu ya hofu kwamba virusi vya homa ya ndege huenda vikakita barani humo.Mpaka sasa mataifa manane yameathiriwa huku visa vipya vikiripotiwa katika mataifa matatu kati yao ya Nigeria,Sudan na Misri.

Virusi vya H5N1 vya homa ya ndege vilisababisha vifo vya zaidi ya watu 150 tangu mwaka 2003 hasa katika mataifa ya Indonesia na Vietnam.Wataalam wana hofu kwamba virusi hivyo huenda vikabadili umbo na kusambaa kati ya wanadamu jambo ambalo huenda likasababisha janga la ugonjwa wa mafua.