1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa India na Afrika wajadili ushirikiano wa biashara na uchumi

Mtullya, Abdu Said8 Aprili 2008

Viongozi wa nchi za Afrika wanakutana mjini New Delhi kujadili njia za kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi baina yao.

https://p.dw.com/p/DeAn
Waziri Mkuu wa India Manmohan Singh.Picha: AP



Mkutano  wa  kihistoria  wa viongozi  wa India na  nchi za Afrika umeanza leo mjini New Delhi kujadili njia za kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kibalozi baina  ya mabara  yao.


Viongozi wasiopungua 15  kutoka  nchi za  Afrika wanahuhduria mkutano huo wa   siku mbili ambapo pamoja  na wenyeji wao wa India wanajadili njia  za kuimarisha uhusiano wa  kiabiashara na kiuchumi.

Mkutano huo ni muhimu kwa kutambua kwamba  biashara  baina  ya   India  an nchi za  Afrika  sasa  imefikia thamani ya dola bilion 30.

Biashara baina ya  pande  hizo imekuwa inaongezeka  tokea mwaka 2001.

Kwenye mkutano wao viongozi  wa  India na Afrika pia watajadili ushirikiano katika sekta za nishati  na usalama.

Mkutano huo unafanyika wakati ambapo India, nchi inayoinukia kuwa na nguvu kubwa  za kiuchumi  inahitaji nishati na raslimali zaidi kwa ajili ya uchumi wake unaondelea kustawi kwa kiwango kikubwa.

Biashara  baina ya India na nchi  za Afrika imekuwa  inastawi haraka mnamo miaka  ya hivi karibuni na imeongezeka mara mbili.Pande mbili hizo zinakusudia  kuongeza  zaidi kiwango cha biashara baina  yao ambacho sasa kinafikia thaamni ya dola bilioni 30.

 Akifungua  mkutano huo leo mjini New Delhi waziri mkuu wa India bwana Manmohan Singh  amesema nchi yake inataka kuona karne hii kuwa ni ya watu wa Afrika  na  India wakishirikiana katika juhudi  za kuendeleza  sera za dunia utandawazi.

Waziri mkuu huyo pia ametangaza kupunguza  ushuru  kwa  bidha za Afrika zinazouzwa  nchini India  Amesema India pia itashirikiana na nchi za Afrika katika sekta za kilimo,miundombinu,elimu ,pamoja na mawasiliano ya kisasa.

Na katika  kipindi  cha miaka mitano ijayo India itatoa mikopo  thamani ya dola bilioni 5 na milioi mia nne.

Akizungumza kwenye mkutano  huo rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya kidemokrasi  ya Kongo  amesema katika ushirikiano  wake na nchi zingine mnamo miaka ya  nyuma  Afrika iliambulia maneno matupu.   Rais Kabila amesema Afrika sasa inataka  kuona miradi ya haraka katika maendeleo.