1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa jumuia ya OSCE mjini Madrid

Oummilkheir29 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CUi0

Madrid:

Mawaziri 40 wa mambo ya nchi za nje kutoka mataifa 56 wanachama wa jumuia ya usalama na ushirikiano barani Ulaya –OSCE wanmeanza mkutano wao wa mwaka wa siku mbili katika mji mkuu wa Hispania Madrid. Mkutano huo unatazamiwa kugubikwa na suala la kitisho cha Urusi cha kujitenda na mkataba muhimu wa silaha unaoweka vikomo vya kutengeneza vifaru vya kijeshi,madege ya kivita na silaha nyenginezo nzito nzito kote barani Ulaya. Moscow inasema itajitoa katika makubaliano ya silaha zisizo za kinuklea barani Ulaya hadi ifikapo december 12 ijayo,ili kujibu mipango ya Marekani ya kutega kinga ya makombora katika nchi za Ulaya ya mashariki.Mbali na mada hiyo mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa wa jumuia ya OSCE wataazungumzia pia mpango wa kurefushwa shughuli za jumuia yao huko Kosovo ,nafasi ya Afghanistan na Kasakhstan kuweza kuchaguliwa kua mwenyekiti wa jumuia ya OSCE mwaka 2009.Hispania ndio iliyokabidhiwa jukumu la kuongoza jumuia kwa mwaka mmoja.