1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kanda kutatuwa mzozo wa Sudan

20 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CJV2

Viongozi wa kanda wanapanga kuwa na mkutano wa viongozi kutatuwa mgogoro unaokuwa nchini Sudan uliozushwa kutokana na kujiondowa kwa waasi wa zamani wa kusini mwa Sudan kutoka serikali ya umoja wa kitaifa.

Uamuzi huo umefikiwa katika mazungumzo tafauti nchini Kenya yenye kuwahusisha Rais Mwai Kibaki wa Kenya,Rais Yoweri Museveni wa Uganda,Rais wa utawala wa ndani wa Sudan kusini Salva Kiir na Rais mstaafu wa Kenya Daniel arap Moi.

Moi mjumbe maalum wa amani wa Kenya kwa Sudan amekuwa na mazungumzo na Museveni hapo jana juu ya juhudi hizo ambapo Kenya ni mwenyekiti wa Mamlaka ya Kiserikali ya Maendeleo IGAD.

Kiongozi wa Sudan ya kusini Salva Kiir hapo jana ameishutumu serikali ya Sudan kwa kujiandaa kwa vita na waasi hao wa zamani wa kusini.