1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kilele kuhusu hatima ya nishati ya Diesel

Sekione Kitojo
2 Agosti 2017

Ksatika mkutano wa kilele mjini Berlin matumaini yamechomoza ya kufikiwa makubaliano kuhusu namna ya kupunguza moshi wa magari unaochafuwa mazingira

https://p.dw.com/p/2hadj
Deutschland Dieselgipfel in Berlin | Wissmann, Krüger, Zetsche & Müller
Picha: picture-alliance/dpa/A. Schmidt

Mazungumzo  baina  ya  wanasiasa  wa  Ujerumani  na watengenezaji  wa  magari  bado  yanaendelea  leo,  hata baada  ya  chama  cha  wenye  viwanda  vya  magari  VDA kusema , wamekubali  kupunguza  utoaji  wa  gesi zinazoharibu  mazingira  kwa  kuboresha  programu maalum katika magari  ya  dizeli milioni 5.

Duru zilizoko  karibu  na  majadiliano  hayo  zimesema mazungumzo  hayo  baina  ya  mawaziri  kadhaa, mawaziri wakuu  wa  majimbo  na  wakuu  wa  viwanda  vya  magari bado  yanaendelea  na  yamegawanywa katika  makundi kadhaa.

Hapo  mapema  leo, chama  cha  wenye  viwanda  vya magari  VDA  kimesema  kitaweka  program mpya  ya uedneshaji ingini katika  magari  milioni  5 ili  kufanya mfumo  wa  kuchuja  moshi uweze  kufanyakazi  vizuri zaidi  na  kushusha  utoaji  wa  gesi  zinazochafua mazingira kwa  asilimia  25  hadi  30  katika  magari  hayo.