1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kilele mjini Washington na jeshi la shirikisho kufanyiwa marekebisho

Oumilkher Hamidou13 Aprili 2010

Viongozi wa mataifa 47 wanakutana Washington kuzungumzia namna ya kuhakikisha usalama wa silaha za kinuklea

https://p.dw.com/p/Mv5k
Rais Barack Obama wa MarekaniPicha: AP

Mkutano wa kilele kuhusu silaha za kinuklea mjini Washington na mpango wa waziri wa ulinzi wa serikali kuu ya Ujerumani Karl-Theodor zu Guttenberg wa kulifanyia marekebisho jeshi la shirikisho Bundeswehr ni miongoni mwa mada zilizopewa kipa umbele na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo.

Tuanzie lakini Washington ambako viongozi wa mataifa 47 wanakutana kuzungumzia njia za kuepusha silaha za kinuklea zisiangukie mikononi mwa magaidi.Gazeti la „Leipziger Volkszeitung linaandika:

Hatari ya kuona silaha za kinuklea zikiangukia mikononi mwa magaidi ni miongoni mwa vipa umbele vya utawala war ais Barack Obama.Pengine hali hiyo haitawavutia wale wanaotaka kuyageuza mabomu ya kinuklea yawe ya kisasa nchini Pakistan,warutubisha maadini ya Plutonium nchini Iran,waimla wa Korea ya kaskazini au waficha ukweli wa mambo nchini Israel.Hata hivyo juhudi za rais Obama za kuitisha mkutano wa kupunguza silaha mjini Washington zitawapa shida wale wanaotaka kueneza biashara ya silaha za kinuklea.Kwa hivyo hawakufanya safari ya bure, kansela Angela Merkel na wenzake kuhudhuria mkutano huu wa kilele mjini Washington.Kisicho dhahiri lakini ni suala kwa kiwango gani wanasiasa wa kimataifa wameingiwa na hofu kuhusu wapi vinakutikana vyenzo vinavyoweza kutumiwa kutengenezea silaha za kinuklea ikiwa wakati huo huo hawafanyi chochote kuhusu mabaki hatari ya zana zilizotumika kutengenezea nishati ya kinuklea?

Gazeti la „Cellesche Zeitung“ linaandika

Lengo la Obama kuhakikisha vyenzo vyote vya kurutubisha maadini vikusanywe katika kipindi cha miaka minne ijayo,ni shida kulifikia katika wakati wote ule ambapo mataifa mfano Iran na Korea ya kaskazini yataendelea kupinga.Ikiwa nchi moja tuu katika dunia yetu hii itaachia vyenzo viangukie mikononi mwa watu wasioaminika,basi amani ya dunia itaangia hatarini.Kwa hivyo rais Barack Obama wa Marekani aliyedhamiria kuona silaha za kinuklea zinateketezwa hatua baada ya hatua,anakabiliana na jukumu lisilotekelezeka.

Gazeti la „Badische Zeitung“ linahisi walimwengu wanastahiki kutupia jicho kwengine pia.Gazeti linaendelea kuandika:

Wakumulikwa sio pekee Iran na Korea ya kaskazini,wanaorutubisha maadini ya uranium bila ya ukaguzi.Kitisho kinaweza pia kutokea Urusi na Pakistan ambako ghala zao za silaha za kinuklea si salama vya kutosha.Na kuna walakini pia katika mfumo jumla wa usalama.Kwa mfano upande wa hifadhi ya raia, miale ya nishati ya kinuklea inapovuja .Rais Obama na wenzake wanalijua hilo-lakini kama kasoro hizo zitaweza kuondolewa haraka,hakuna anaeamini,seuze tena baadhi ya nchi zinaliangalia suala la nishati ya kinuklea na bomu la kinuklea kua ni suala linalohusu mamlaka ya ndani ya nchi.Kwa namna hiyo vyenzo hivyo vinaweza kuingia mikononi mwaAl Qaida –na sote tukaingia hatarini.

Dossier 1 Trauerfeier für gefallene Soldaten in Kundus
Maombolezi ya wanajeshi watatu wa Ujerumani waliouliwa Kundus nchini AfghanistanPicha: picture-alliance/dpa

Mada yetu ya mwisho magazetini hii leo inahusu mpango wa waziri wa ulinzi wa serikali kuu ya Ujerumani, kulifanyia marekebisho jeshi la Shirikisho-Bundeswehr.Gazeti la „Hannoversche Allgemeine Zeitung“ linaandika:

„Uchunguzi bila ya miko,ndio anaoutaka waziri wa ulinzi Karl-Theodor zu Guttenberg kutoka halmashauri ya miundo mbinu aliyoiunda.Jeshi jumla la shirikisho,kuanzia jana linajikuta katika hali ya kufanyiwa uchunguzi kwasababu linatakiwa litekeleze shughuli zake bora zaidi,bila ya gharama kubwa na liwe la kimambo leo zaidi.Waziri wa ulinzi amegusia ndipo hasa anapohimiza mageuzi.Wanajeshi wamekua wakilazimika kila siku kutumia vifaa ambavyo vyengine vimetengenezwa hata kabla wenyewe hawajazaliwa.Kinachoudhi zaidi ni kwamba hali hiyo imekua ikijulikana tangu zamani.Rudolf Scharping aliwahi kuunda halmmashauri kama hiyo mnamo mwaka 1999 na kuongozwa na rais wa zamani wa shirikisho Richard von Weizsäcker.Kwa kina na bila ya miko,ilielezwa miaka kumi iliyopita,nini kinahitaji kufanyiwa marekebisho katika jeshi la shirikisho na vipi linaweza kugeuzwa liwe la kisasa.Tunachowaombea wanajeshi ni kuona angalao safari hii mpango huo hautomalizikia ndani ya matoto ya meza.

Mwandishi:Hamidou, Oummilkheir/Dt.Agenturen

Mpitiaji:Mohammed Abdul-Rahman