Mkutano wa kilele wa Afrika na Ufaransa kuanza kesho
5 Desemba 2013Matangazo
Hivi leo Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Laurent Fabius, anakutana na wenzake wa mataifa hayo ya Afrika katika mkesha wa mkutano huo wa kilele, ambao miongoni mwa nchi zinazohudhuria na zikipewa umuhimu mkubwa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo kimsingi haina mafungamano ya kihistoria na Ufaransa. Jee kwa nini ikawa hivyo?
Mohammed Khelef amezungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe, ambaye alipitia Ujerumani akiwa njiani kuelekea Paris, mwanzoni mwa wiki hii.
Kusikiliza mahojiano hayo, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mahojiano: Mohammed Khelef/Benard Membe
Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman