1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kilele wa EU.

Halima Nyanza(ZPR)28 Oktoba 2010

Mkutano wa siku mbili wa kilele, wa Wakuu wa Umoja wa Ulaya unaanza leo mchana, mjini Brussels, Ubelgiji.

https://p.dw.com/p/Pqkc
Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy, akiwa na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel.Picha: picture alliance/abaca

Mkutano huo unafanyika wakati, Ujerumani na Ufaransa zinakabiliwa na upinzani mkali kwa kutaka kwao mabadiliko katika mkataba wa Lisbon wa umoja huo.

Jana, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alitetea pendekezo la kutaka kuwepo kwa adhabu kali dhidi ya mataifa ya sarafu ya Euro yatakayoshindwa kufikia viwango vya mkataba wa Umoja wa Ulaya katika uthibiti wa uchumi.

EU Gipfel in Brüssel
Viongozi kutoka nchi za Umoja wa Ulaya.Picha: AP

Kansela Merkel anajiandaa kufanyia marekebisho mkataba wa sasa wa Lisbon kwa ajili ya kuweza kukabiliana na matatizo yatakayotokea baadaye kuhusiana na madeni.