1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kilele wa G8 kuanza Camp Dave

Admin.WagnerD18 Mei 2012

Rais wa Marekani Baracka Obama anamkaribisha leo katika ikulu ya White House Rais mpya wa Ufaransa, Francois Hollande kabla ya viongozi hao wawili kujiunga na wenzao katika mkutano wa kilele wa nchi tajiri ulimwenguni G8

https://p.dw.com/p/14xKs
Am Randes des G8-Gipfels in Washington haben sich die Außenminister der USA und Russlands, Clinton und Lawrow (links) auch zu bilateralen Konsultationen getroffen. - US Secretary of State Hillary Clinton (R) and Russian Foreign Minister Sergei Lavrov (L) prepare to hold a bilateral meeting at Blair House in Washington DC, April 12, 2012. The officials are wrapping up two days of talks during the G-8 Foreign Ministers Meetings. REUTERS/Mike Theiler (UNITED STATES - Tags: POLITICS) eingestellt von: ml
Außenminister-Treffen der G8 in WashingtonPicha: Reuters

Rais Obama analenga kuimarisha uhusiano wa Marekani na Ufaransa na kisha kisha kuishinikiza Ulaya kujitahidi zaidi katika kutatua mgogoro wa kiuchumi unaoendelea kushuhudiwa katika eneo hilo.

Francois Hollande, aliyeapishwa mapema wiki hii kama rais mpya wa Ufaransa, tayari ameibua hisia kali kwa kupinga mpango wa Ulaya wa kubana matumizi na kusema kuwa ataviondoa vikosi vya Ufaransa kutoka Afghanistan ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Obama kumhimiza Hollande

Obama mwenye umri wa miaka 50 huenda akautumia mkutano wake wa utangulizi katika ofisi yake kumhimiza Hollande mwenye umri wa miaka 57, Msoshalisti kutathmini upya mipango yake ya Aghanistan ambayo imeiweka Ufaransa katika ratiba ya kuondoka nchini humo mapema kuliko washirika wake wengine wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO.

Viongozi wanaoziwakilisha nchi za G8 katika mkutano unaopangwa kuanza Camp Dave
Viongozi wanaoziwakilisha nchi za G8 katika mkutanowa kilele unaopangwa kuanza Camp DavePicha: picture-alliance/dpa

Lakini viongozi hao wawili ambao wameleezea uungaji mkono wao kwa sera za ukuaji wa kiuchumi barani Ulaya, wanatarajiwa kuwa na msimamo wa pamoja kuhusu mzozo wa madeni unaoukumba ukanda unaotumia sarafu ya euro, ambao huenda ukaugubika mkutano wa mwishoni mwa wiki wa kundi la nchi nane tahiri zaidi ulimwenguni.

Utawala wa Obama ulitumia fedha nyingi kupambana na mdororo wa uchumi wa mwaka wa 2007-2009, na Hollande analenga kuutumua mpango wa kubana matumizi kwa kupitia uwekezaji wa kubuni nafasi zaidi za ajira.

Mkutano wa kilele wa G8 unajiri wakati Wagiriki wakiendelea kuondoa pesa kwenye akaunti zao kutokana na kuongezeka hofu kwua nchi hiyo itaondoka katika kanda ya sarafu ya euro, na masoko ya hisa yameingiwa hofu kuhusu uwezekano wa kuibuka mgogoro mkubwa wa kiuchumi ulaya.

Mzozo wa Ugiriki wazua hofu

Obama na maafisa wenginwa Marekani wamewataka maafisa wa Ulaya kufanya juhudi za kuimarisha ukuaji uchumi katika eneo hilo, wakihofia kuwa hali hiyo huenda ikaathiri uchumi wa Marekani na kutishia nafasi za Obama kuchaguliwa zena katika uchaguzi wa tarehe nane Novemba. Ikulu ya White House iliuhamisha mkutano wa G8 hadi Maryland badala ya Chicago, kama njia moja ya kuepuka maandamano wakati Rais wa Urusi Vladimir Putin akitarajiwa kuhudhuria.

Suala la mgogoro wa deni la Ugiriki linatarajiwabkupewa kipau mbele
Suala la mgogoro wa deni la Ugiriki linatarajiwabkupewa kipau mbelePicha: picture-alliance/dpa

Waziri wake Mkuu Dimtry Medvedev atahudhuria badala yake pamoja na wenzake wa G8 wanaohudhuria kwa mara ya kwanza kama vile Francois Holande, Mario Monti wa Italia, na Yoshihiko Noda wa Japan, pamoja na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na Stephen Harper wa Canada. Wengine ni Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Obama wa Marekani, rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barosso, na Rais wa Baraza kuu la Umoja wa Ulaya Herman van Rompuy.

Huo ndio utakaokuwa mkunao mkuwba zaidi wa kilele kuandaliwa katika eneo la Camp Dave ambalo lilijengwa katika miaka ya tisini na linajulikana kama sehemu ya ilikofanyika mazungumzo yaliyopita ya amani ya mashariki ya kati.

Mwandishi: Bruce Amani/Reuters
Mhariri: Josephat Charo