1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Kilele wa ILO wafanyika Geneva

30 Mei 2016

Wajumbe katika Mkutano wa Kimataifa wa Shirika la Wafanyakazi Duniani, ILO, wanatakiwa kufikia makubaliano ya kimataifa yatayoshurututisha kisheria ulinzi wa haki za binaadamu katika mfumo mzima wa uzalishaji duniani.

https://p.dw.com/p/1IxJO
Picha: SEDOAC

Ripoti ya shirika la haki za binadamu iliyotolewa Jumatatu (30.05.2016) ni mahsusi kwenda sambamba na kuanza kwa mkutano huo wa ILO ambayo inahimiza kutungwa kwa kanuni ambazo zitalazimisha kisheria kulindwa kwa haki za binaadamu na makampuni ya kibiashara.

Serikali, waajiriwa na wafanyakazi kutoka duniani kote wanakutana mjini Geneva kwa mkutano wa kilele wa wafanyakazi wa kila mwaka unaoanza Jumatatu hadi Juni 10 kujadili namna ya kuhakikisha kunakuwepo "kazi za heshima " katika mfumo mzima wa kazi duniani kuanzia bidhaa inapoanza kuzalishwa hadi inapomfikia mteja, halikadhalika utowaji wa huduma.

Ripoti ya kurasa 21 ya shirika la haki za binaadamu la Human Rights Watch imezingatia utafiti wake wa miongo miwili kuhusu ajira ya watoto na ukiukaji mwengine wa haki za wafanyakazi, uharibifu wa mazingira, ukiukaji wa haki katika masuala ya afya, ardhi, chakula na maji chini ya mfumo mzima wa uzalishaji na utowaji huduma duniani.

Mamilioni wateseka na ukiukwaji wa haki za binaadamu

Julianne Kippenberg, mkurugenzi msaidizi wa haki za watoto katika Human Rights Watch, anasema mamilioni ya watu duniani wanateseka kwa ukiukaji wa haki za binaadamu kwa sababu ya hatua mbaya za makampuni ya kibiashara na kanuni dhaifu za serikali na kwamba taratibu zitakazoshurutisha kisheria ni njia pekee yenye uhalisia kuhakikisha kwamba makampuni haiwanyonyi wafanyakazi na au kuchangia ukiukaji wa haki zao.

Wafanyakazi katika machimbo ya mawe India.
Wafanyakazi katika machimbo ya mawe India.Picha: Getty Images/AFP/C. Mao

Kippenberg amesema "Sheria zilioko katika kulinda haki za binaadamu katika mfumo mzima wa uzaslishaji hadi bidhaa inapomfikia mteja hazitosi.Kile hasa tunachokitarajia katika mkutano chama cha wafanyakazi duniani unaoanza mjini Geneva utachukuwa uamuzi wa kuwa kufikia mkataba utakaotekelezwa kisheria na kuzilazimisha serikali kuratibu biashara kuhusiana na ulinzi w ahaki za binaadamu katika suala mfumo mzima wa uzalishaji."

Ripoti yao imeangazia ukiuakaji mbali wa haki za binaadamu katika dhana ya mfumo wa mzima wa uzalishaji bidhaa duniani kama vile uvunjaji wa haki za wafanyakazi na mbinu za kivikandamiza vya wafanyakazi viwandani wenye kutengeneza nguo na viatu kwa walaji duniani, watoto kutumikishwa katika mazingira hatari ya mashamba ya tumbaku inayonunuliwa na makampuni ya kimataifa ya kutengeza sigara, ukiukaji mbaya sana wa haki za wahamiaji wanaofanya kazi katika sekta ya ujenzi ajali mbaya zinazogharimu maisha kwa wanamigodi wenye ujuzi wanaochimba dhahabu kwa ajili ya soko la kimataifa.

Udhaifu wa sheria

Shirika la haki za binaadamu la Human Rights Watch limegunduwa kwamba mara nyingi serikali zinashindwa kutimiza wajibu wa kulinda haki za binadamu kwa kupitia taratibu zenye ufanisi katika shughuli za kibiashara:

Ishara ya kutumikishwa kwa watoto.
Ishara ya kutumikishwa kwa watoto.Picha: picture-alliance/dpa

Kippenberg anasema "Tunaona kwamba kanuni za hiari vile zilivyo hazitoshi kulinda haki zaidi ya watu milioni 450 wanaofanya kazi katika mfumo wa uzalishaji na utowaji huduma duniani."

Miongozo ya kanuni za Umoja wa Mataifa katika suala la biashara na haki za binaadamu ni kanuni za kimataifa ambapo utekelezaji wake sio wa kisheria na zinataka kampuni zenyewe zihakikishe kwamba haki za binadamu zinaheshimiwa katika shughuli zake.

Mwandishi: Mohamed Dahman/HRW Report

Mhariri: Mohammed Khelef