1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mafashisti mamboleo wawasili mjini Cologne.

Mtullya, Abdu Said19 Septemba 2008

Mkutano wa kupinga uislamu unatarajiwa kuanza kesho mjini Cologne.

https://p.dw.com/p/FLUW
Wapinzani wa mkutano wa mafashisti mamboleo mjini Cologne.Picha: picture-alliance/ dpa


Wajumbe  wenye  itikadi kali za kibaguzi wameanza kuwasili  leo mjini Cologne kuhudhuria mkutano  wa  kupinga  hasa ujenzi  wa msikiti katika mji huo.

Wajumbe hao kutoka sehemu mbalimbali  za  bara la  Ulaya wanahudhuria mkutano huo uliotayarishwa na  chama cha kinachopinga kuenezwa kwa uislamu .

Habari zinasema polisi wengi wamepelekwa  katika mji wa Cologne ili kuzuia mapambano baina ya  wabaguzi hao na watu wanaowapinga.


Mkutano huo umeandaliwa na chama kinachopinga  kinachoitwa  kuenea  kwa dini ya kiislamu.

Wakati huo huo mamia ya watu walishikama mithili  ya mnyororo mbele ya sehemu  ambapo msikiti  unatarajiwa kujengwa, katika sehemu ya Ehrenfeld, kupinga mkutano wa wawakilishi  wa itikadi kali za mlengo wa kulia.

Meya wa sehemu hiyo, Josef Wirges 

ameushutumu mkutano  huo.

Akizungumzia  juu ya harakati  za kupinga  mkutano wa wabaguzi, mbunge wa  chama  SPD kwenye  bunge la mji wa Cologne Lale Akgün amesema jitihada hizo zinaonesha kuwa mji wa Cologne umesimama  wima dhidi  ya mafashisti mamboleo.

Jumuiya  ya waislamu wa kituruki inayojenga msikiti  huo imesema maandamano ya kupinga mkutano  wa wabaguzi  yamethibitisha  mtazamo  wa stahamala  miongoni mwa  wakaazi wa mji wa Cologne  ambapo watu wa nasaba mbalimbali za  kitamaduni wanaishi.  

Hatahivyo  meya  mkuu  wa  mji huo Fritz Schramma amesema  stahamala huondoka  ikiwa  mipaka fulani inavukwa.  Ameeleza  kuwa  ameshiriki katika maandamano ya  kupinga mkutano wa mafashisti mamboleo kwa sababu mji wake hautaki  kuona mkutano kama huo.

Chama kinachojiita  kuwa  kinatetea maslahi ya watu  wa mji wa  Cologne Pro Cologne  kimewaalika  mafashisti mamboleo kuhudhuria mkutano unaoanza  kesho katika mji huo ,kwa lengo la kupinga  wanachoita kuenezwa uislamu.

Mafashisti mamboleo wanapanga kufanya mkutano mkubwa wa hadhara hapo kesho mjini Cologne

Wawakilishi wa makanisa,vyama vya wafanyakazi na asasi za kiraia pia wanajiandaa kupinga mkutano  huo.

Katibu mkuu wa  baraza kuu la waislamu nchini Ujerumani  bwana Aiman Maziyek amewataka waislamu wote washiriki katika harakati za kupinga mkutano huo ,leo  na kesho katika mji wa Cologne

Kamishna  wa masuala ya wahamiaji nchini Ujerumani bibi Maria Böhmer pia ametoa mwito wa  kupinga mkutano wa mafashisti  mamboleo unaotarajiwa kuanza kesho  mjini Bonn.