1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi magazetini

Oumilkher Hamidou13 Desemba 2010

Maridhiano yaliyofikiwa Cancun yamesifiwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hata kama hakuna anaelazimishqwa kuyatekeleza

https://p.dw.com/p/QWr1
"Cancun Can"-Cancun inaweza wanasema waandamanaji hao waliofurahishwa na maridhiano yaliyofikiwa.Picha: DW/Jeppesen

Mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi mjini Cancun na shambulio la kigaidi mjini Stockholm ni miongoni mwa mada zilizotangulizwa mbele na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo.

Tuanzie lakini Cancun ambako walimwengu wanaonyesha wameridhika na matokeo ya mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi ikilinganishwa na hali namna ilivyokuwa mkutano kama huo ulipomalizika mwaka mmoja uliopita mjini Copenhagen.Gazeti la "Badische Neueste Nachrichten" linaandika:"Ufanisi wa mkutano huu ni ile hali kwamba haijawa kazi bure.Utaratibu uliowekwa na Umoja wa mataifa unaweza kuendelea.Jumuia ya kimataifa imeahidi kuendelea kupambana na mabadiliko ya tabia nchi-japo kama ni kwa hatua ndogo ndogo na kila mmoja kwa upande wake.Lengo hilo la awamu mbili limekubaliwa hata na wachafuzi wakubwa wa mazingira,Marekani na China.Kinachokosekana lakini ni masharti bayana na ya lazima kwa kila nchi kupunguza kiwango maalum cha moshi wa sumu unaotoka viwandani."

Hata gazeti la "Sächsische Zeitung" linazungumzia juu ya ufanisi hata kama una walakin."Ukilinganishwa na mkutano wa kilele wa Copenhagen mwaka mmoja uliopita,huu wa Cancun umeweza kuleta mafanikio.Wakati ule,utaratibu wa kuhifadhi tabia nchi ulikuwa nusra uvunjike.Hivi sasa lakini utaratibu huo umejipatia msukumo.Lakini hata kama maridhiano yanatia moyo:kuna baadhi ya mambo ambayo si bayana na wala si shuruti.Hifadhi ya tabia nchi inahitaji makubaliano ambayo nchi zote za dunia zitayafuata,nchi maskini zitasadiwa kulinda tabia nchi na viwango maalum kuweka vya kupunguza moshi wa sumu unaotoka viwanda ni.Na zaidi kuliko yote kuhakikisha kwamba Marekani na China,madola mawili yanayochafua zaidi hali ya hewa,hayaendelei kupinga kila kinachofikiwa.

Nalo gazeti la "Main-Post" linaandika:"Kuna habari nzuri kutoka Cancun:Nchi 193 kati ya 194 za jumuia ya kimataifa zinakubaliana na lengo la kuhakikisha hali jumla ya hewa inapanda kwa digrii mbili na kuwa sawa na hali namna ilivyokuwa mna mo mwaka 1850-yaani kabla ya enzi za viwanda.Na Bolivia ilikuwa nchi pekee iliyopinga waraka huo kwasababu inahisi haujenda mbali mno-kwasababu inaamini hata kiwango hicho cha digree mbili za hali ya ujoto kinaweza kuwa na madhara kwa baadhi ya mataifa.Mataifa mengine mfano wa Japan,na hasa Marekani na China yangetaka pengine kuzuwia maridhiano hayo yasifikiwe-lakini hazikuwa na njia.

Explosion einer Autobombe in Stockholm Schweden
Gari limeripuliwa mjini Stockholm December 11 mwaka huu-dakika chache baadae,mtu mmoja akajiripua mita chache tuu karibu na eneo hio hilo la mji mkuu.Picha: picture-alliance/dpa

Mada yetu ya pili magazetini inahusu shambulio la kigaidi katika mji mkuu wa Sweeden Stockholm.Gazeti la "Neue Osnabrücker Zeitung" linaandika:" Taifa linaloamua kupambana na ugaidi katika nchi za nje,na kupigania demokrasia iimarishwe,linabidi lijue tuu kwamba litakabiliana na upinzani,tangu ugenini kwenyewe mpaka nyumbani.Inabidi iwe tayari kukabiliana na hali kama hiyo.Njia bora ya kinga,tena kupita sheria yoyote ya usalama,ni kupunguza juhudi hizo na kuelezea kila mara aina na msingi wa harakati za kijeshi ili kuepusha dhana za majivuno ya kiuchumi na kitamaduni.Hiyo ndio njia bora-kama sio njia pekee ya kudumu kuweza kupata amani.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mpitiaji:Abdul-Rahman,Mohammed