1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa maendeleo wa umoja wa mataifa umemalizika bila ya makubaliano

12 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2t

Umoja wa Mataifa –New-York:

Mkutano wa Umoja wa mataifa kuhusu maendeleo ya kudumu kwa kutilia maanani nishati isiyochafua mazingira umemalizika bila ya kufikiwa masikilizano mjini New-York.Waziri wa mazingira wa serikali kuu ya Ujerumani Sigmar Gabriel amekataa kutia saini waraka wa mwisho wa mnkutano huo kwa niaba ya Umoja wa ulaya.Waraka huo unadhoofisha maakubaliano yaliyofikiwa awali mna unatoa ishara mbaya ,amesema waziri Sigmar Gabriel akihalalisha msimamo wa nchi za umoja wa ulaya.Uswisi imeunga mkono msimamo huo na kuyataja matokeo ya mkutano huo kua hayana maana.