1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa umoja wa Ulaya

1 Machi 2007

Mawaziri 27 wa ulinzi wa Umoja wa ulaya wanakutana jana na leo mjini Wiesbaden,Ujerumani kuzungumzia maswali ya ulinzi.

https://p.dw.com/p/CHJA
Kikosi maalumu cha Bundeswher
Kikosi maalumu cha BundeswherPicha: AP

Mawaziri hao wanataka kukuza ushirikiano na shirika la ulinzi la magharibi NATO na Umoja wa Mataifa.Mada nyengine mkutanoni ni hali nchini Afghanistan na sera za silaha za Umoja wa Ulaya.

Mawaziri wa ulinzi muda mrefu sasa wamekuwa wakiwekwa kando katika duru za mawaziri wa Umoja wa ulaya.Hasa Uingereza haikutaka kuona UU unajitokeza mno kushindana na NATO chini ya uongozi wa Marekani katika maswali ya ulinzi.

Ndio sababu mawaziri wa ulinzi hawakuwa wakichukua sehemu muhimu.Hali hii sasa imebadilika: Kila kukicha hivi sasa Umoja wa Ulaya unajaribu kujitambulisha kwa mkakati wake binafsi wa kijeshi:

„“Naamini, chnazo cha badiliko hili ni vita vya kienyeji katika Balkan.Kwavile sote tuliona ni aibu kushindwa kumaliza umwagaji damu huko.“

Hivyo ndivyo anavyosema mbunge wa Umoja wa Ulya karl von Wogau wa chama cha CDU anaeongoza tume ya maswali ya ulinzi ya bunge la ulaya.Ingawa Bunge la ulaya halina sauti katika maswali ya ulinzi,hatahivyo huangalia matokeo kwa makini.

Idadi ya wanajeshi wa UU katika Bosnia-Herzegovina –ambyako uingereza imetangaza hivi punde kuondoa majeshi yake iliopeleka huko- imepangwa kuyapunguza kutoka kima cha 6.000 na kubakisha 2.500.UU lakini utakabia kuwa macho kuangalia kinachopita huko.

Mkoani Kosovo UU unapanga kutumia polisi kusimamia utaratibu wa kutoa mamlaka ya ndani kwa mkoa huo.Katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo,vikosi vya UU vilisimamia uchaguzi uliopita.Jumla ya opresheni 14 za kijeshi au mchanganyiko wa kijeshi na kiraia zilifanyika ndani na nje ya Ulaya chini ya paa la sera za pamoja za kigeni na ulinzi.

UU hauna vikosi vyake maalumu bali hutegemea wsanachama kuchangia majeshi.Hivi sasa lakini unaunda kikosi maalumu kinachoitwa (Battle-group)-vikosi vya vita .Kikosi hiki kina askari 1.500 kinachotumika kuzima moto panapozuka mapigano mfano Afrika.

Ushirikiano mkubwa zaidi unapiganiwa uwepo pia katika maswali ya silaha na zana za kijeshi.Na mbunge wa chama cha CDU katika bunge la Ulaya Karl von Wogau anasisitiza:

„Kwamba nchi 27 zanachama wa Umoja wa Ulaya zinatumia Euro bilioni 170 kwa mwaka kwa shughuli za ulinzi.Tuna wanajeshi milioni 2.Tuna vifaru 10.000 na ndege za kivita 3.000.“

Katika kikao hiki cha Wiesbaden, swali moja linasubiri kupatiwa jibu:Wapi upo mpaka unaoitenganisha Umoja wa Ulaya na Shirika la NATO ?

Swali hili lazuka kwavile, sehemu kubwa ya nchi zanachama wa UU ni wanachama pia wa shirika la ulinzi la magharibi-NATO.Marekani kwahivyo, inahofia wingi kama huo wa nchi za UU, shirika la NATO huenda likawa halina maana kuwapo.