1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa misaada ya maendeleo wamalizika.

Duckstein, Stefanie (DW Afrika-Nahost) / Accra NEU5 Septemba 2008

Misaada ya kimataifa ya maendeleo ilifanikiwa, lakini ilikuwa kidogo na wakati mwingine hata ilipopatikana haikuleta tija ya kutosha.

https://p.dw.com/p/FBwp
Kijana kutoka nchini Nigeria akiandika katika ubao wakati wa masomo katika kijiji cha Tibiri, hali inayoeleza umuhimu wa kupatiwa misaada ya maendeleo katika bara la Afrika.Picha: picture-alliance/ ZB



Msaada wa kimataifa wa maendeleo umekuwa kidogo , usiofaa ama pia ulipotolewa wa kutosha haukuweza kuleta maendeleo ya kutosha. Hayo yamesemwa na wajumbe zaidi ya 1,000 kutoka mataifa fadhili na yale yanayopokea misaada ambao wamekuwa wakijadili utendaji wa pamoja katika shughuli za misaada ya maendeleo. Jana Alhamis mkutano wa tatu wa mawaziri unaohusu misaada ya maendeleo ulimalizika. Matokeo ni mabadiliko katika azimio la Paris la mwaka 2005, na kuwa kile kinachoitwa sasa mpango wa utekelezaji wa Accra.



Ni maridhiano , hakuna cha zaidi , lakini ndio maridhiano, kwamba imepatikana hati hiyo ya msingi , kwamba utendaji wa pamoja wa kuleta maendeleo umekuwa mzuri, hii ina maana ya hali bora. Kile kinachofahamika kama mpango wa utekelezaji wa Accra ulikamilishwa katika mji mkuu wa Ghana Accra na mawaziri kutoka mataifa fadhili na mataifa yanayoendelea. Hata hivyo kwa Eckhard Deutscher , ambaye ni mkuu wa kamati ya maendeleo ya shirika la maendeleo ya kiuchumi, OECD, makubaliano hayo ya Accra ni mbinu za ubabaishaji.


Kila mmoja anafahamu , kwamba hati hiyo ya maridhiano ni kitu gani. Nimefurahi kama mwenyekiti wa kamati ya misaada ya maendeleo, kuwa tumefika mbali kwa kufikia makubaliano hayo. Hata kama naona mapungufu. Lakini nina wajumbe wote katika kamati yangu ambao tunaweza kurekebisha, ni wapi pana vikwazo , ni mtazamo gani wanao dhidi ya mabunge ya nchi zao, dhidi ya umma, na dhidi ya serikali zao. Hili lazima nilifanye na siwezi kulidharau.



Kwa upande wa mataifa ya Marekani na Japan yanasitasita kuchukua jukumu la kuweka muda maalum wa kutoa misaada yao. Hali hii ingezirahisishia nchi zinazoendelea kuweza kupanga miradi yao ya maendeleo pamoja na bajeti. Kumi Naidoo kutoka katika asasi isiyo ya kiserikali ya harakati dhidi ya umasikini nchini Afrika kusini anasema kuwa hilo sio tatizo pekee, ambalo linakwamisha azimio hilo.


Kwa upande wa lugha , tunaweza kuwapa alama za juu. Kwa upande wa muda maalum wa kuchukua hatua tunawapa alama za chini kabisa. Kwanza kwa upande wa kujua ni lini misaada itapatikana tulikuwa tunajitahidi kuzisukuma nchi fadhili kuwa na msimamo wa kuzifanya nchi zinazoendelea kufahamu kile wanachoweza kutarajia katika muda wa miaka mitatu hadi mitano.


Na kwa upande wa suala muhimu zaidi, amesema Naidoo, ni utaratibu wa kupeleka fedha hizo. Misaada ya nchi fadhili mara nyingi inatolewa kwa masharti, kwamba nchi inayopewa msaada ni lazima ikubali masharti kadha ya nchi fadhili. masharti hayo anasema Naidoo ni pamoja na kutumia wataalamu wa nchi inayotoa misaada, unapaswa kutumia makampuni kadha kutoka nchi fadhili, na wanajaribu kukushawishi kubadilisha baadhi ya sera za nchi ambazo hazileti maana yoyote.



►◄