1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa OSCE .

2 Desemba 2010

Mkutano wa OSCE kukamilika hii leo.

https://p.dw.com/p/QNj4
Rais wa Kazakhstan Nursultan Nazarbayev, na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel.Picha: AP

Viongozi wa dunia wametoa wito wa pamoja wa kuwepo shirika lenye nguvu la usalama na ushirikiano Ulaya, OSCE, katika mkutano wa kwanza wa shirika hilo tangu mwaka 1999 nchini Kazakhstan.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel  amesema shirika hilo lenye wanachama 56 lazima kwanza lihakikishe amani na uhuru inakuwepo katika mipaka yake. Akiigusia  nchi mwenyeji, Merkel amesema hakikisho la haki za binaadamu na uhuru wa kujieleza na wa vyombo vya habari, ni lazima utekelezwe.

OSZE Gipfel in Kasachstan NO FLASH
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Rodham Clinton,na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel katika mkutano wa OSCE.Picha: AP

 Kazakhstan ni nchi ya kwanza ya iliyokuwa muungano wa Sovieti  kushikilia uwenyekiti wa shirika hilo. Waandishi wa habari wasio na mipaka wamesema nchi hiyo haifai kuandaa mkutano huo kwani haifikii viwango vya shirika hilo.

OSCE liliundwa wakati wa vita baridi kama njia ya majadiliano kati ya mataifa ya kikomyunisti na Magharibi.

Mwandishi Maryam Abdalla/DPAE